Home KITAIFA TPSF NA TCCIA YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA 

TPSF NA TCCIA YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA 

Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Bodi ya Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) leo wakutana kujadili namna bora ya kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi wa Taifa letu.

Mkutano huu umetokana na maelekezo aliyotoa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akihutubia mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara Tarehe 09 Juni 2023, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Raisi, alielekeza Sekta Binafsi nchini kujitathmini ueendeshaji wake na kuhakikisha kuwa mabaraza ya biashara ya mikoa na Wilaya yanaimarika.

Akizungumza kwenye kikao hiki Bi. Angelina Ngalula, Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha vyama vya Biashara nchini vinaratibiwa ipasavyo ili kuleta ufanisi.
“Nchini kuna zaidi ya vyama 2000 vya biashara (Private Sector Organisations-PSO’s) vidogo na vikubwa na idadi hiyo inaendelea kukua. Hii inaashiria kuwa Sekta Binafsi nchini inakuwa kwa kasi na ni muda muafaka kuwepo na usimamizi mzuri wa vyama hivi ili kuhakikisha vyama vinaendeshwa kwa ufanisi. ” alisisitiza Bi. Ngalula.

“Tunafahamu TCCIA imekasimia majukumua ya kuendesha mabaraza ya biashara ya mikoa na Wilaya. Lakini kama tulivyomsikia mheshimiwa raisi, bado tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha mabaraza haya yanafanyika kwa wakati lakini pia wajumbe wa mabaraza wawe na sifa za kushahuri serikali kwenye ngazi zote”. aliongeza bi Ngalula.

Kwa upande wake, Bw. Edmund Mkwawa, kaimu raisi wa TCCIA, alilisisitiza juu ya umuhimu wa umoja wa sekta binafsi katika kuhakikisha Sekta Binafsi inakua.

“Tusikubali kugawanyika kwa maslahi ya watu wachache, kama viongozi wa Sekta Binafsi tuna jukumu kubwa la kuhakikisha vyama vyetu vinahimarishwa na kufanya kazi kwa pamoja. Jukumu letu liwe kuhakikisha Sekta Binafsi ya Tanzania, inakuwa shindani yenye kuleta ajira, kipato na kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla wao”. alisema Bw. Mkwawa.

TPSF na TCCIA wamedhamiria kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa manufaa mapana ya nchi.

Kama muendelezo wa maelekezo ya Mhe. Raisi, TPSF itaiitisha kikao maalum na wakuu wa vyama vyote vya biashara nchini ilikujadili na kupendekeza mwongozo wa sekta binafsi nchini na kukubaliana mfumo sahihi wa kuratibu vyama hivyo.

TPSF ni chama mwavuli wa vyama vya biashara nchini na mwaka huu itakuwa inasherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake 1998.

Previous articleWALIOORODHESHWA KWENYE REA III KUPATA UMEME KABLA YA 2024 MBEYA VIJIJINI
Next articleWAJANE NCHINI WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA MSAADA WA KISHERIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here