Home KITAIFA TPA YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA TOZO MPYA ZA BANDARI NCHINI

TPA YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA TOZO MPYA ZA BANDARI NCHINI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wa usafirishaji majini na wavuvi Jijini Mwanza katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji hilo lengo ikiwa ni kukusanya maoni ya wadau juu ya maombi ya mapitio ya tozo mpya yaliyowasishwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Afisa Mkuu wa Masoko Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania Robert Soko amesema,wanatarajia mabadiliko ya tozo mpya za bandari nchini kuleta unafuu kwa watumiaji wa bandari pamoja na kuleta tija katika bandari ili kuendana na mabadiliko ya biashara sambamba na mabadiliko ya uchumi yanayojitokeza.

Kaimu Mkurugenzi mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nahson Sigala amesema, wanaendelea kuchukua maoni ya maombi ya marekebisho ya tozo mpya za bandari kwa njia ya barua ambapo kwa mkoa Mwanza yanapokelewa katika ofisi za Mamlaka hiyo na mwisho wa kuchukua maoni ni Juni 20 mwaka huu.

“ Tumewashirikisha wadau mbalimbali ili kupokea maoni kutoka kwao ya maombi ya marekebisho ya tozo mpya za bandari zilizowasilishwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA ) kwakua wao ni wadau wakubwa katika masuala ya usafirishaji majini na tunategemea maoni ambayo wameyatoa yatasaidia kuboresha tozo hizo, Robert Soko,” Afisa Mkuu wa Masoko Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania.

Previous articleWIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, FEDHA KUSHIRIKIANA KUELIMISHA JAMII
Next articleDKT. BITEKO ATOA SIKU 14 KUANZA UZALISHAJI WA ALMASI MWADUI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here