Home KITAIFA TPA KUJENGA GATI JIPYA NA ONE STOP CENTER MTWARA

TPA KUJENGA GATI JIPYA NA ONE STOP CENTER MTWARA

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Juma Kijavara, amesema kwa mwaka ujao wa fedha TPA inatarajia kutangaza tenda kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Gati jipya eneo la Kisiwa Mgao Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, kwa ajili ya kuhudumia shehena ya mzigo mchafu.

Akizungumza leo Juni 22, 2023 Mkoani Mtwara katika kikao cha wadau wa Bandari ya Mtwara, Kijavara, amesema ujenzi huo utaenda sambamba na ujenzi wa kituo cha pamoja cha kutoa huduma (One Stop Center) cha kuhudumia wafanyabiashara.

Kikao hicho kimefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanafi Msabaha, ambaye ameeleza mpango wa serikali wa kujenga reli kutoka Mtwara itakayoenda mpaka Ruvuma katika Bandari ya Mbamba Bay.

Previous articleMBUNGE NJEZA AZIDI KUPAMBANIA BARABARA ZA JIMBONI KWAKE
Next articleMABAKI YA ALIYEPOTEA 2022 YAKUTWA PORINI MOROGORO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here