Home KITAIFA TIMU YA WAKUFUNZI MPIRA WA MIGUU DPA YATWAA UBINGWA POLISI JAMII CUP

TIMU YA WAKUFUNZI MPIRA WA MIGUU DPA YATWAA UBINGWA POLISI JAMII CUP

Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi-Dar es salaam.

Mashindano ya Polisi Jamii Cup yaliyofanyika katika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) yamefikia tamati huku timu ya wakufunzi wa Chuo hicho wakiibuka washindi kwa kutwaa kombe katika mpira wa miguu dhidi ya timu ya wanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi.

Mbali na mchezo huo fainali nyingine ilikuwa ya kuvuta kamba kati ya wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi ambapo wanafunzi wa kozi ya uofisa ilishinda mchezo huo.

Mgeni rasmi katika Mashindano hayo kamishna msaidizi wa Polisi ACP Mairi Makori amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Pollisi Nchini IGP Camillus Wambura kwa namna ambavyo ameendelea kutoa dira ya maboresho ya Polisi Jamii katika kuileta jamii karibu na Jeshi hilo.

Amewataka askari hao wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi kuilewa vizuri dhana ya Polisi Jamii katika kutokomeza vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali hapa Nchini ambapo amewashauri kuandaa michezo kama hiyo katika maeneo yao ya kazi mara baada ya mafunzo yao kukamilika.

Kwa Upande wake afisa mnadhimu namba Moja (SO1) katika chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DAP) kamishna msaidizi wa Polisi ACP Obadia Nselu amebainisha kuwa lengo la Mashindano hayo ni kuonyesha kwa vitendo jinsi jamii na Polisi wanavyokutana na kubadilishana taarifa mbalimbali za uhalifu na wahalifu katika Jamii.

Kocha wa timu ya wakufunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es. Salaam (DPA) mrakibu wa Polisi SP Silvesta Shilikale amesema kuwa walijiandaa vyema na Mashindano hayo kitendo kilichopelekea kuibuka na ushindi huo.

Sambamba na hilo mchezaji wa timu ya wakufunzi chuoni hapo Sajenti SGT Gaston Komba amesema ushindi huo ni kutokana na maelekezo mazuri ya kocha wao ambaye alipanga safu ya mashambulizi zaidi katika lango la timu ya wanafunzi wa kozi ya mkaguzi msadizi wa Polisi na kupelekea kutwaa kombe pamoja na medali mbalimbali.

Pia Kocha wa Timu ya wanafunzi wa kozi ya uofisa katika mchezo wa kuvuta kamba mwanafunzi wa kozi ya uofisa Rogatus Nyoni amesema siri ya ushindi wao ni mbinu na maandalizi mazuri waliyoyafanya.

Nae Mchezaji wa timu ya wanafunzi wa kozi ya mkaguzi wa Polisi Yasin Mohamed amesema wameyapokea matokeo hayo ambapo amebainisha kuwa wanajipanga upya kwa mashindano mengine ili kutwaa ubingwa.

Previous articleWAZIRI MHAGAMA AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA WATENDAJI WA CHAMA
Next articleRAIS SAMIA AONGOZA VIKAO VYA UONGOZI WA CCM NGAZI YA TAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here