Home KITAIFA THRDC YASAINI MKATABA NA P.I.A KUWEZESHA SHUGHULI ZA KIRAIA NA WATETEZI WA...

THRDC YASAINI MKATABA NA P.I.A KUWEZESHA SHUGHULI ZA KIRAIA NA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umesaini mkataba na Shirika la Protection International Afrika wenye thamani ya Euro laki moja na themanini.

Mkataba huo wa mwaka mmoja umelenga kusaidia kukuza nafasi za kiraia nchini kwa kuimarisha ushiriki wa Makundi yote ya Watetezi wa Haki za Binadamu (USAWA).

Shughuli ambazo zinatarajiwa kutekelezwa kwenye mradi huo zitasaidia kutachangia moja kwa moja kwenye utekeleza wamalengo ya Mpango mkakati mpya wa Mtandao wa mwaka 2023- 2027.

Katika makubaliano hayo ambayo yamesainiwa rasmi tarehe 14, Aprili mwaka huu na utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mapema Mei na kumalizika Desemba 31, 2023.

Katika mkataba huo wanufaika wake ni Watetezi wa Haki za Binadamu bara na visiwani wakiwemo watetezi wa haki za wanawake, watu wenye ulemavu na jamii za kifugaji.

Mradi huo unatarajiwa kuongeza nguvu katika utetezi wa haki za binadamu nchini kwa kuboresha mazingira yenye usawa kwa jamiii nzima.

Previous articleJESHI LA POLISI SONGWE LAKEMEA USHOGA, UKATILI
Next articleWIZARA KUANZISHA MINADA NA MAONESHO YA MADINI YA VITO NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here