Home KITAIFA THBUB YALIVALIA NJUGA SAKATA LA AJALI YA NAIBU WAZIRI DUGANGE NA KIFO...

THBUB YALIVALIA NJUGA SAKATA LA AJALI YA NAIBU WAZIRI DUGANGE NA KIFO CHA MWANAFUNZI UDOM

 

TUME ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Imetangaza kuanza rasmi uchuguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Nusura Hassan Abdallah,aliyefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospital ya Faraja Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza leo Mei 10 jijini Dodoma Mwenyekiti wa Tume Hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema kwa kipindi cha hivi karibuni tume ya haki za Binadamu na utawala bora imeona katika vyombo vya habari zikihusisha ajali ya Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI, Dkt Festo dugange na kifo cha Nusura Abdallah .

Jaji Mstaafu Mwaimu amesema taarifa hizo za vyombo vya habari zimeonekana kukinzana kutokana na taarifa zilizotolewa na jeshi la Polisi,Chuo kikuu cha Dodoma , Hospitali ya Faraja iliyopo Himo Mkoani Kilimanjaro na taarifa za wananchi kupitia mitandao ya kijamii.

 

Aidha Jaji Mstaafu Mwaimu amesema Tume inapoona kumetokea mashaka kutoka kwa wananchi kuhusu jambo lolote linaloashiria uvunjwaji wa haki za binadamu au mashaka ya haki kutokutendeka ina mamlaka ya kufanya uchuguzi juu ya jambo hilo.

Previous articleMAKAMBA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA KUTEKELEZA MRADI WA LNG
Next articleSIRRO AAGWA RASMI LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here