Home KITAIFA TGNP KUADHIMISHA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA KWA STYLE YA AINA YAKE, YAJA...

TGNP KUADHIMISHA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA KWA STYLE YA AINA YAKE, YAJA NA TAMASHA LA KITAIFA LA JINSIA (GENDER FESTIVAL)

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi (wa tatu kushoto-mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha TGNP na wahariri kuhusu ujio wa Tamasha la Jinsia (Gender Festival) na maadhimisho ya miaka 30 ya TGNP kilichofanyika Septemba Mosi, 2023
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akitoa wasilisho kuhusu maadhimisho ya miaka 30 ya TGNP na ujio wa Tamasha la Jinsia lake wakati wa kikao kazi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) Septemba Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam
Bi. Rose Mwalongo akielezea usuli kuhusu Tamasha la Jinsia 2023 mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Septemba Mosi, 2023
Amin Mgeni, ambaye ni Mhariri kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuhusu ujio wa Tamasha la Jinsia (Gender Festival) na maadhimisho ya miaka 30 ya TGNP

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika majadiliano

 

Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakichangia mada wakati wa kikao kazi cha Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi (wa tatu kushoto-mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha TGNP na wahariri kuhusu ujio wa Tamasha la Jinsia (Gender Festival) na maadhimisho ya miaka 30 ya TGNP kilichofanyika Septemba Mosi, 2023

 

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), asasi hiyo imeandaa shughuli kadhaa kusherehesha maadhimisho hayo.

Moja ya shughuli ni uwepo wa Tamasha la Kitaifa la Jinsia (Gender Festival) ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 07 Novemba hadi tarehe 10 Novemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa Septemba Mosi, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi Lilian Liundi katika kikao kazi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kilichofanyika katika ofisi za TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, tamasha hilo litawaleta wadau mbalimbali wanaotetea masuala ya jinsia pamoja.

Akizungumzia kuhusu ujio wa tamasha la kitaifa la Jinsia (Gender Festival) , Lillian amesema kufanyika kwa tamasha hilo utakuwa ni mwendelezo wa matamasha mbalimbali yaliyoandaliwa na asasi hiyo kuanzia mwaka 1996.

“TGNP imekuwa ikifanya matamasha mbalimbali kuanzia mwaka 1996 ,na hadi kufikia sasa tumeshafanya matamasha 15 ya kitaifa , na Tamasha la Jinsia (Gender Festival ) litakalofanyika Novemba 07 hadi 10, mwaka huu litakuwa ni tamasha la 15 kufanyika” alisema Lillian na kuongeza.

“Mada kuu katika tamasha hilo litakuwa ni Miaka 30 ya TGNP na Tapo la Ukombozi wa Wanawake na katika mada hii kitu kikubwa tutakachokiangalia ni safari yetu TGNP ya tangu tulipoanza hadi sasa”

Kando na mada hiyo, mada nyingine zitakazaojadiliwa ni pamoja na Nyayo Zetu, Urithi Wetu”, “Zaidi ya Miaka 30 ya Tapo la Ukombozi wa Wanawake, Dira yetu, Ndoto Yetu

Akiongea katika kikao kazi hiko kuzungumzia usuli wa Tamasha la Jinsia 2023, Rose Mwalongo amesema, lengo la tamasha hilo ni kushirikishana ujuzi, uzoefu na kusherehekea mafanikio katika masuala ya jinsia na familia na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kusonga mbele pamoja na kujenga uhusiano.

Akiongea kwa niaba ya wahariri, Amin Mgeni kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) amesifu jitahada zinazoendelea kufanywa na TGNP katika harakati za kupambania usawa wa kijinsia pamoja na namna wanavyoendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya jinsia na hata ile dhana ya usawa wa kijinsia ni kwa ajili ya mwanamke pekee sasa inatoweka.

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ulianzishwa mwaka 1993 ikiwa ni miongoni mwa taasisi za mwanzo kabisa zinazotetea haki za binadamu, wanawake na kikubwa zaidi  masuala ya usawa wa kijinsia

Previous articleRAIS SAMIA AWAAPISHA WAZIRI NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI
Next articleJINSI NILIVYOSHINDA MILIONI 20 ZA BAHATI NASIBU KWA URAHISI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here