Home KITAIFA TFS,TAWA NA TANAPA SIMAMIENI VYEMA MAENEO YA UHIFADHI

TFS,TAWA NA TANAPA SIMAMIENI VYEMA MAENEO YA UHIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa, ameziagiza mamlaka za uhifadhi nchini, kusimamia vyema maeneo ya hifadhi yaliyotengwa kwa shughuli za utalii ili kufikia lengo wizara hiyo kukusanya shilingi trioni 14 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mchengelwa amesema hayo mkoani Morogoro katika maonesho ya 30 ya kilimo,mifugo na uvuvi Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani humo.

Pia amesisitiza uwajibikaji kwa bidii katika kutangaza vivutio vya utalii ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa wawindaji wazawa huku akiitaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuongeza jitihada katika kudhibiti ubadhirifu wa upotevu wa fedha na utoaji wa vibali vya usafirishaji mkaa kwa pikipiki.

Previous articleBENKI YA NMB YATENGA SH. BILIONI 20 MRADI WA BBT
Next articleMAOKOTO CHEMKA WILAYANI HAI YAZIDI KUPANDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here