Home MICHEZO TFF YAPONGEZWA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MICHEZO KIGAMBONI

TFF YAPONGEZWA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MICHEZO KIGAMBONI

 

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya michezo zikiwemo Hosteli, ofisi na viwanja vya michezo ambavyo vitaendeleza michezo hapa nchini.

Mhe. Mwinjuma ametoa pongezi hizo leo Aprili 15, 2023 Wilayani Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Elimu, Utamaduni na Michezo.

 

Amesema Sekta ya Michezo nchini Tanzania katika kipindi cha hivi karibuni imepata mafanikio makubwa katika medani za Kimataifa kwa Timu za Tanzania kushiriki mashindano ya Kimataifa yakiwemo ya AFCON ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa michezo kutokana na ushiriki ano mzuri kati ya Serikali na wadau wa Sekta Binafsi.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia ameieleza Kamati hiyo kuwa TFF inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa viwanja vya michezo na hosteli ili kuziwezesha timu za Taifa kufanya vizuri zaidi pia kuendeleza vipaji vya vijana hapa nchini.

Ameongeza kuwa TFF itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuimarisha michezo.

Previous articleAKAMATWA KWA TUHUMA YA KUZALISHA NA KUSAMBAZA DAWA BANDIA
Next articleKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU, UTAMADUNI NA MICHEZO YATEMBELEA BMT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here