Mei 28, 2023 TETE FOUNDATION imeungana na jamii kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani, ambapo taasisi hiyo imefanya maadhimisho hayo katika kituo na shule Amani iliyopo Mvomero – Mkoa wa Morogoro
Katika maadhimisho hayo Mkurungezi wa TETE FOUNDATION, Bi. Suzana Senso amesema takwimu inayoonesha mtoto wa kike kukosa darasani siku 5 -7 kwa kushindwa kujisitiri kutokana na kuwa kwenye hedhi, mwaka huu Taasisi yetu imekuja na dhima *”Sitakosa Shule Campaign”* ambapo mwaka huu tunagawa taulo za kike za kutumia kwa muda wa miezi 6 kwa mabinti zaidi ya 50 waliopo kwenye shule ya Amani
Shukurani za kipekee kwa wadau walioshirikiana na TETE FOUNDATION kufanikisha hili zoezi ikiwemo UAP INSURANCE TANZANIA kwa kuwa sehemu ya kufanikisha zoezi hili bila kusahau wazalishaji wa taulo za kike za HQ PAD na Ministry ya “love of Christ Ministry” kwa kuwa sehemu ya kuhakikisha kila mtoto wa kike wa Shule ya Amani hakosi darasani kwa muda wa miezi 6 kutokana na kuwa kwenye hedhi