Home KITAIFA TEITI KUJA NA MPANGO MKAKATI WA KUWAKOMBOA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI TANZANIA

TEITI KUJA NA MPANGO MKAKATI WA KUWAKOMBOA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI TANZANIA

 

Kaimu Meneja kitengo cha Uwazi na Uwajibikaji TEITI, Mhandisi. Joseph Kumburu amesema, Katika ripoti ya kipindi cha mwaka 2019/20 jumla ya kampuni 31 zilitoa takwimu za ajira ambapo katika kampuni hizo Watanzania walikuwa 7,804 na wageni ni 550,hii inaonesha kuwa ajira kwa watanzania ni asilimia 93 ya waajiriwa wote katika migodi hiyo 31 na wageni ni asilimia 7.

Aidha Kumburu amesema, wameanza kufanya tafiti mbalimbali za namna bora ya kuwahusisha wachimbaji wadogo katika ripoti za Taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika Raslimali za madini,mafuta na gesi asilia ( TEITI ) ili Kufanya tafiti mbalimbali za namna wananchi wanavyonufaika na Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini,

 

Pia kuanzisha mfumo wa kielektroniki utakaotumiwa na kampuni pamoja na Taasisi za Serikali kuripoti malipo yaliyofanywa na kampuni za uchimbaji wa madini kwa Serikali.

Kumburu ameongeza kuwa, TEITI itaendelea kuhakikisha Serikali inaweka mifumo ya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia nchini ili kuboresha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa rasilimali za madini nchini ikiwa na lengo la kufikia kiwango cha asilimia 10 ya Pato la Taifa kama Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (5).

Hatahivyo amesema,matarajio ya TEITI ni kuwa kitovu cha kutoa taarifa za madini, mafuta na gesi asilia kuhusisha taarifa na malipo ya mazingira katika ripoti zake kwa kuweka wazi majina ya wamiliki wa hisa katika Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia ikiwa pamoja na kuweka wazi mikataba ambayo Serikali imeingia na Kampuni za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Previous articleDKT. MPANGO ATUA NCHINI BURUNDI
Next articleDC AAGIZA KILA KAYA KUFUGA KUKU WASIOPUNGUA WATANO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here