Home KITAIFA TEA YATOA UFADHILI WA MILIONI 500 KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU

TEA YATOA UFADHILI WA MILIONI 500 KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU

 

 

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa ufadhili wa shilingi Milioni 500 kwaajili ya mradi wa ukarabati wa miundombinu pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunza katika vyuo viwili vya elimu ya juu vilivyopo Tanzania na Zanzibar.

 

Pia shule 8 za wanafunzi wenye mahitaji maalum zimewezeshwa madarasa 10 ikiwemo matundu 50 ya vyoo pamoja na mabweni matatu yanayozingatia mahitaji yao na mamlaka hiyo

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa (TEA) Bahati Geuzye Agosti 10,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya (TEA).

Amesema kuwa katika ufadhili huo Taasisi ya karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST) ilipokea ufadhili wa shilingi Milioni 200 na chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kampasi ya Benjamin Mkapa iliyopo Pemba kilipokea ufadhili wa shilingi Milioni 300 ambapo ufadhili huo umenufaisha wanafunzi 700 katika vyuo hivyo viwili.

“Kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa TEA inafadhili miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu na kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kujifunza na kufundishia katika ngazi zote za elimu Kwa Tanzania Bara na ngazi za elimu ya juu Kwa Tanzania Zanzibar,”amesema.

Mbali na hayo,amesema kuwa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaoratibiwa na TEA katika mwaka wa fedha 2022/23 shilingi Bilioni 10.99 ziligharimu ufadhili wa miradi 132 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.

“Miradi hiyo ilijumuisha ujenzi wa madarasa 114 katika shule 38 za msingi 36 na sekondari 2,maabara 10 za Sayansi katika shule 5 za sekondari,matundu ya vyoo 888 katika shule 37 za msingi 29 na sekondari 8,

Miundombinu kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na utoaji wa vifaa vya kujifunza na kufundishia katika shule 8 za msingi , miundombinu hiyo imehusisha Ujenzi wa madarasa 10,matundu ya vyoo 50 na mabweni 3 kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu,”amesema.

Hata hivyo katika mwaka wa fedha 2023/24 mamlaka ya Elimu Tanzania imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 8 kwaajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Amesema kiasi hicho Cha fedha kitatumia kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari katika Maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara miradi hiyo itakapokamilika itanufaisha wanafunzi 39,484 na walimu 169 katika shule za misingi na sekondari.

“Miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na Ujenzi wa madarasa 82,matundu ya vyoo 336,mabweni 10,Ujenzi wa maabara 18 za masomo ya Sayansi na nyumba za walimu 32,

Pia katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Mfuko wa Elimu wa Taifa utatoa ufadhili kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu na kuwezesha Ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika taasisi moja ya elimu ya juu Tanzania-Zanzibar,”amesema.

TEA ni taasisi ya umma inayofanyakazi chini ya Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia,TEA ilianzishwa Kwa sheria ya bunge ya Mfuko wa Elimu Na.8 ya mwaka 2001 chini ya kifungu 5(1) pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2013 Kwa lengo la ukarabati uendeshaji wa mfuko wa Elimu.

 

Previous articleSHIRIKA LA UTU KWANZA LAANDAA MBIO ZA KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA WANANCHI WANAOKOSA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA, WAFUNGWA NA FAMILIA ZAO
Next articleDC ILEJE AWATAKA WAMAMA KUTENGA MUDA KUWANYONYESHA WATOTO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here