Home KITAIFA TCRA YAENDELEA KUWATAHADHARISHA WATUMIAJI WA LAINI ZA SIMU

TCRA YAENDELEA KUWATAHADHARISHA WATUMIAJI WA LAINI ZA SIMU

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA ), Dkt. Jabir Bakari ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuhakiki laini zao za simu mahususi wanazotumia ili kupunguza wimbi kubwa la utapeli (tuma kwa namba hii) unaondelea na kuwaumiza wananchi.

Ametoa Rai hiyo julai 18, 2023 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na waandishi wa Habari.

Amesema utapeli unaondelea unahusisha laini za simu ambazo tayari zimesajiliwa na hazijafanyiwa uhakiki ikiwa ni pamoja za watu ambao walishapoteza maisha ‘’kweli kwamba mwanzo ulikuwa unaenda kuchukua kadi na kitambulisho chochote baadae tukasema kwamba uwe umsajiliwa ,baadae tukasema lazima uwe unatumia dole gumba ,baadae tukaona zile simu kadi zinatumika nawatu ambao siyo wenyewe na wanakuwa Zaidi ya mtu mmoja,’’.

Hata hivyo Dk. Bakari amesema kuwa takwimu zinaonyesha kwamba mikoa mitano inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika hadi Juni 2023 ni pamoja na Dar es Salaam ambapo una Laini Milioni 11,797,544.

Pia Mwanza Laini 4,246,212, Arusha laini 3,858,283,Mbeya laini 3,687,622 na Dodoma laini 3,421,006.

Amesema kuwa gharama za muunganisho wa simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimekuwa zikipungua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2015 gharama zilikua ni TZS 30.58 na kwa sasa gharama zilizokokotolewa ni TZS 1.86 kwa dakika.
“ Hii inachangia kupunguza gharama za rejareja za upigaji wa simu na kuondoa ulazima wa wateja kuwa na simu zaidi ya moja”amesema.

Ameendelea kufafanua kuwa TCRA imeendelea kutoa Leseni na kusimamia masharti ya leseni kwa watoa huduma za mawasiliano nchini,ambapo hadi kufikia Juni 2023, tunawatoa huduma 1481 na jumla ya leseni 2,415.

Dkt. Jabir amesema TCRA imefanya ukaguzi kwa watoa huduma 671 wa simu na intaneti, utangazaji na posta ili kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni.

“Upimaji wa hivi karibuni ulifanyika kuanzia mwezi Aprili hadi Juni, 2023 umehusisha makampuni (06) ya simu katika maeneo ya miji saba (07) ambayo ni Kahama, Songwe, Mbeya, Kigoma, Katavi, Tabora, na Rukwa.

Previous articleAWESO AMUONDOA MKANDARASI MRADI WA MAJI KAZURAMIMBA; AAGIZA MWEZI MMOJA WANANCHI WAPATE MAJI
Next articlePOLISI ADAKWA NA MIHADARATI AKUTWA NA MAGUNIA MANNE KWENYE GARI_ MAGAZETINI LEO JUMATANO JULAI 19/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here