Home KITAIFA TAWA YAPONGEZWA KWA KUENDELEZA UTALII WA MALIKALE

TAWA YAPONGEZWA KWA KUENDELEZA UTALII WA MALIKALE

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja leo ametembelea banda la wizara ya maliasili kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara yake katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam na kuipongeza mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kuendeleza utalii wa malikale

Pongezi hizo zimeelekezwa kwa taasisi hiyo kwa jitihada za dhati katika kuboresha miundombinu ya utalii katika maeneo hayo, kwa kununua boti la kisasa linalotoa huduma kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya magofu ya kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.

Pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika hifadhi hiyo, Mhe. Mary Masanja pia ameipongeza TAWA kwa kazi nzuri ya kuhamasisha watanzania kutembelea hifadhi hiyo ambapo watalii wengi wa ndani wameonekana wakifanya safari nyingi za utalii katika hifadhi hiyo.

Pia Mhe. Mary ameipongeza TAWA kwa kuunganisha Utalii wa malikale, Wanyamapori na bahari kitu ambacho kinatoa wigo mpana kwa kufanya shughuli zao za kitalii katika maeneo mbalimbali yenye vionjo tofauti vya utalii ambapo kwa kufanya hivyo watalii wanaongeza idadi ya siku za kukaa katika nchi yetu na hivyo kuongeza kipato.

Previous articleHUJUMA , UPIGAJI VYABAINIKA NHIF_ MAGAZETINI LEO JUMATANO JULAI 12/2023
Next articleMBUNGE SUBIRA MGALU ATOA ELIMU NA UFAFANUZI WA VIFUNGU MKATABA WA BANDARI, AONYA UBAGUZI DHIDI YA RAIS SAMIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here