Home KITAIFA TAWA YAFANYA SEMINA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KUHUSU USIMAMIZI WA...

TAWA YAFANYA SEMINA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KUHUSU USIMAMIZI WA PORI LA AKIBA KILOMBERO

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanya semina na kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma juu ya usimamizi wa pori la akiba Kilombero

Semina hiyo imefanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Bunge,kwa lengo kuieleza Kamati ya kudumu ya bunge juu ya umuhimu wa pori la akiba Kilombero, changamoto zinazokabili pori hilo na namna TAWA ilivyojipanga kukabiliana na changamoto hizo.

Akizungumza wakati wa kutoa wasilisho mahsusi la pori la akiba Kilombero, Kamishna wa Uhifadhi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Joas Makwati,amesema Pori hilo lina umuhimu mkubwa kwa Taifa kwani linachangia asilimia sitini na 65 ya maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere (JHPP) ambayo yanatarajia kuzalisha Megawati 2, 115 za umeme utakaotumika majumbani, viwandani na kwenye shughuli za usafirishaji.

Sambamba na faida hiyo, pori hilo limedaiwa kuwa chachu ya kufungua fursa za utalii ikiwemo shughuli za uwindaji wa kitalii ambazo zinaongeza fedha nyingi za kigeni ikizingatiwa kuwa mpaka sasa pori la akiba Kilombero lina Vitalu vinne vya uwindaji wa kitalii.

Makwati amesema katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi 2020/21 TAWA ilitoa jumla ya shilingi 425, 221,402 Kwa Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi kama gawio la 25% ya mapato yatokanayo na shughuli za utalii katika pori la akiba Kilombero.

Previous articleSIRRO AAGWA RASMI LEO
Next articleWAZIRI MKUU AZINDUA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI ULOTO BENJAMIN MKAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here