Home KITAIFA TANZANIA, ZAMBIA NA CHINA KUSHIRIKIANA UFUFUAJI TAZARA

TANZANIA, ZAMBIA NA CHINA KUSHIRIKIANA UFUFUAJI TAZARA

 

 

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akifuatilia majadiliano yaliyofanyika kati yake na Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Zambia Frank Tayali, Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian kwa njia ya matandao kuhusu kuboresha utendaji na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akifuatilia majadiliano yaliyofanyika kati yake na Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Zambia Frank Tayali, Balozi wa China Nchini Tanzanai, Mhe. Chen Mingjian kwa njia ya matandao kuhusu kuboresha utendaji na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Ally Possi wakifuatilia majadiliano yaliyofanyika kati ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarwa, Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Zambia Frank Tayali, Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian (hawapo pichani) kwa njia ya mtandao kuhusu kuboresha utendaji na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli unaimarishwa kwa kutenga fedha kila mwaka ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo ya ndani na nje ya Tanzania inayosafirishwa upitia Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza katika Kikao cha Utatu kilichojumuisha Balozi wa China, Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Tanzania na Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Serikali ya Zambia kilichofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma, Waziri Mbarawa amesema kuimarisha kwa usafiri wa reli wa nchini hususani Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kutapunguza changamoto za usafirishaji wa mizigo hususani kwa mizigo inayokwenda Zambia na Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

“Kufanyika kwa kikao ni utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya Rais wa Tanzania na Zambia katika kuhakikisha TAZARA inafufuliwa upya na hapa tumejadiliana njia bora zaidi za kulifufua upya ambapo tayari kamati zilizoundwa zinaendelea na kazi na zitawasilisha ripoti kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi’ amesema Waziri Mbarawa.

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa kwa sasa tayari kamati tatu zimeshaundwa ili kujadili namna bora ya kuimarisha Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuhakikisha shirika hilo linasafirisha mzigo mwingi zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa China chini, Mhe. Chen Mingjian amesema Serikali ya china kama sehemu ya mdau mkubwa wa reli hiyo iko tayari kuhakikisha shirika hilo linaboreshwa ili kutoa mchango kwa nchi na kurahisisha usafirishaji wa mizigo.

Naye Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Zambia Mhe. Frank Tayali amemuhakikishia Waziri Mbarawa na Balozi Chen kuwa Zambia imejipanga na tayari kama sehemu ya mbia wa Shirika hilo inaendelea kutekeleza makubaliano mbalimbali yaliyoingiwa baina ya Tanzania na Zambia lengo likiwa kulifufua upya shirika hilo.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akifuatilia majadiliano yaliyofanyika kati yake na Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Zambia Frank Tayali, Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian kwa njia ya matandao kuhusu kuboresha utendaji na Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Ally Possi

Previous articleMEYA NDILE :CHANDARUA SIO ZA KUVULIA SAMAKI
Next articleWABUNGE WACHARUKIA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA _ MAGAZETINI LEO IJUMAA SEPTEMBA 08/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here