Home KITAIFA TANZANIA NA MALAWI ZAKUBALIANA UJENZI WA MRADI WA UMEME MTO SONGWE

TANZANIA NA MALAWI ZAKUBALIANA UJENZI WA MRADI WA UMEME MTO SONGWE

Waziri wa Nishati January Makamba (kulia) na Waziri wa Nishati wa Malawi, Ibrahim Matola (kushoto) wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo wakati wa Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 11, 2023.
Waziri wa Nishati January Makamba (kulia) na Waziri wa Nishati wa Malawi, Ibrahim Matola (kushoto) wakionesha hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo wakati wa Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 11, 2023.
Waziri wa Nishati wa Malawi Ibrahim Matola (katikati) akiteta jambo na Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam
Ujumbe wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Nishati Jaruary makamba( aliyeketi kulia) na  Waziri wa Nishati wa Malawi, Ibrahim Matola Mtawalia ( aliyeketi kushoto), wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika Sekta ya Nishati, Agosti 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
Viongozi Wakuu kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake,kutoka kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania Mhandisi Decklan Mhaiki (TANESCO), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania( TPDC), Mussa Makame(pili kushoto), Kamishna wa Umeme  Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga (tatu kushoto)na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka( pili kulia) wakimsikiza Waziri wa Nishati Januari Mkamba( hayupo pichani), wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika Sekta ya Nishati, Agosti 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi katika Sekta ya Nishati, Agosti 11, 2023 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Decklan Mhaiki (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini Malawi (ESCOM) Kamkwamba Kumwenda (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya mashirika hayo, wakati wa Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 11, 2023.

 

 

Na Zuena Msuya, DSM

Waziri wa Nishati wa Tanzania January Makamba na Waziri wa Nishati wa Malawi Ibrahim Matola wamesaini hati za makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Nishati kwa kuanza Ujenzi wa Mradi wa kufua umeme katika Mto Songwe.

Hati ya Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam, Agosti 11, 2023, na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati nchini Malawi, Mhandisi Alphonso Chikuni.

“Makubaliano hayo ni matunda ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili ambapo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alifanya ziara nchini Malawi na Rais wa Malawi, Dkt. Lazarus Chakwera alifanya ziara nchini  Tanzania ambapo katika mazungumzo yao walisisitiza kuongeza mashirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwamo sekta ya nishati ili kuimarisha maendeleo kutokana na kukua kwa sekta hiyo”, alisema Makamba.

Amesema kuwa Mashirikiano hayo yamelenga maeneo makubwa matatu ambayo ni kuzalisha kwa pamoja umeme wa Megawati 180  kwa kutumia maporomoko ya Maji ya Mto Songwe ambao umepita pande zote za nchi hizo.

Ushirikiano katika utafiti, utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi na tatu ni Ushirikiano kwenye eneo la ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme katika nchi hizo mbili.

Makubaliano mengine ni kujenga miundombinu ya kuunganisha Gridi za nchi hizo kwa lengo mahsusi la kuwa Gridi moja Kusini mwa Afrika.

Aidha tayari Makubaliano hayo yameweka utaratibu wa ushirikiano kwa kuunda Kamati ya pamoja ya ngazi ya Mawaziri, Kamati ya Wataalam ili kufuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo.

Kila nchi itateuwa wataalam wake ndani ya kipindi cha Mwezi mmoja, sambamba na hilo mwezi Octoba mwaka huu vikao vya kuanza utekelezaji wa makubaliano hayo vitaanza.

Amesema mpaka sasa Tanzania inamiradi kadhaa ya kuinganisha nchi hiyo na nyingine ambapo tayari iko katika hatua za mwisho kukamilisha manunuzi ya ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha Tanzania na Zambia ambayo itaenda mpaka ukanda Kusini mwa Afrika, vilevile Zambia imeunganisha Gridi yao na nchi ya Msumbiji.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Malawi, Ibrahim Matola alimshukuru Waziri Makamba kwa kukubali ushirikiano huo na kuhakikisha makubaliano hayo yanafikiwa.

“Matola alisisitiza kuwa makubaliano hayo yataimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi zao mbili ambao umedumu kwa muda mrefu, pia yatawezesha wananchi wa mataifa hayo kuwa karibu zaidi na kuimarisha uchumi wao”, alisisitiza Matola.

Alisema huo utakuwa mradi wa kwanza wa ushirikiano wa sekta ya nishati kati ya Malawi na Tanzania ambapo nchi hizo zitagawana sawa megawati za umeme zitakazozalishwa ambapo kila nchi itapata Megawati 90.

Alieleza kuwa kwa sasa nchi hiyo itafanya ukarabati wa njia ya kusafirisha umeme kutoka mji wa Lilongwe hadi mpakani mwa Tanzania na Malawi, kwa kuwa nchi hiyo inauhitaji mkubwa wa nishati hiyo kwa kuzingatia kuwa umeme ndiyo muhimili  wa maendeleo ya uchumi.

Ujumbe huo kutoka Malawi ulipata fursa ya kutembelea Kituo cha kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia cha Kinyerezi na kituo cha Kupokea Gesi Asilia kutoka Lindi na Mtwara ili kujionea namna shughuli za uzalishaji zinavyofanyika.

Hafla ya utiaji saini wa hati za makubaliano ya ushirikiano katika ya Sekta ya Nishati ilitanguliwa na kikao cha majadiliano kwa ngazi ya wataalam baadaye Makatibu Wakuu kilichofanyika Agosti 9 na 10, 2023.

 

 

Previous articleHARRY KANE ASAINI RASMI FC BAYERN MUNCHEN.
Next articleWAJASIRIAMALI WASOMI TUNDUMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA UWEZESHAJI KIUCHUMI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here