Home KITAIFA TANTRADE NA UCSAF KUTOA HUDUMA YA MAWASILIANO (WIRELESS INTERNET-Wifi) ) KATIKA UWANJA...

TANTRADE NA UCSAF KUTOA HUDUMA YA MAWASILIANO (WIRELESS INTERNET-Wifi) ) KATIKA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA

 

Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote( UCSAF) wamekutana na kufanya kikao cha jinsi ya kutoa huduma ya mawasiliano ya interneti WiFi (Wireless Internet) kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J.K Nyerere kwa kipindi chote cha Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (almaarufu Maonesho ya SabaSaba) yatakayofanyika kuanzia tarehe 28 Juni – 13 Julai, 2023.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 08 Juni 2023, katika Ofisi za TanTrade Dar es Salaaam kwa lengo la kuboresha na kurahisisha miundombinu ya mawasiliano ili kuwasaidia washiriki pamoja na watembeleaji kuweza kupata mawasiliano kwa njia rahisi na haraka zaidi katika kipindi chote cha Maonesho hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Bw. Fortunatus Mhambe, Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara, TanTrade kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bi. Latifa M. Khamis ameishukuru Taasisi ya UCSAF kwa kutoa huduma hiyo inayolenga kurahisisha mawasiliano na kuboresha Maonesho yawe na mvuto zaidi.

‘Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, natoa shukrani zangu za dhati kwa Taasisi ya UCSAF kwa kukubali kuboresha huduma za internet katika kipindi cha Maonesho, hivyo tunapenda kuuhabarisha Umma kwamba katika Maonesho hayo, huduma za Internet zitakuwa zimeimarishwa na kuboreshwa kwa ajili ya watembeleaji na waoneshaji na kuwarahisishia kuonesha biashara zao kwa njia rahisi zaidi’ alisema.

Naye Mratibu kutoka UCSAF – Kanda ya Pwani Bw. Baraka Elieza amesema kuwa Taasisi ya UCSAF itahakikisha kuwa huduma za Internet zinakuwa nzuri na zenye kuleta tija katika Uwanja wa Maonesho na kuwafanya waoneshaji pamoja watembeleaji kuweza kufurahia huduma hizo kuanzia tarehe 28 Juni – 13 Julai, 2023.

Previous articleNAIBU CAG ZANZIBAR AAPISHWA
Next articleMALALAMIKO YA UNYANYASAJI WA MWEKEZAJI KWA WANANCHI YAMFIKIA DC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here