Home KITAIFA TANROADS YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KATIKA DHANA NA KANUNI ZA USIMAMIZI WA...

TANROADS YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KATIKA DHANA NA KANUNI ZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA SERIKALI

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila akiongea na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila akiongea na viongozi na mameneja wa TANROADS ambao wanapatiwa mafunzo ya kuongezewa uwezo mkoani Morogoro Aprili 25, 2023 

Viongozi na Mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Wamepatiwa mafunzo ili kuwaongezea uwezo, kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akifungua Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro leo jumanne April 25-203 Mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema takwimu zinaonesha kuwa Tanroads ina viongozi wapya ambao wanahitaji kujengewa uwezo kwenye uongozi na hata wale walioteuliwa zamani wanahitaji kukumbushwa kuhusu masuala ya uongozi ili kutimiza malengo ya serikali ya Rais Samia ambaye ameweka mkazo katika kuboresha miundombinu ya barabara na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Amesema pia mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi wa Wakala katika dhana na kanuni za usimamizi wa rasilimali za serikali kwa lengo la kuboresha utendaji wao wa kazi na kuendelea kutoa huduma bora kwa watanzania na kufikia malengo yaliyopangwa.

“Mafunzo haya yanayotolewa na wawezeshaji waliobobea katika masuala mbalimbali ya uongozi katika Serikali na yanagusa masuala muhimu ya uongozi wa umma ikiwemo utawala bora, usimamizi wa masuala ya fedha, ununuzi, usimamizi wa rasilimali watu, maadili ya uongozi, utunzaji wa siri za serikali, mawasiliano, Itifaki za serikali, utunzaji wa nyaraka za serikali na masuala mengine mengi ya Kiuongozi” Amesema.

Viongozi na mameneja wa TANROADS wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila wakati akifungua mafunzo ya siku 5 ya kuwaongezea uwezo viongozi na mameneja wa TANROADS nchini

Amesisitiza kuwa ni matarajio yake kuwa mafunzo hayo yataleta matokeo chanya ikiwemo kuongeza tija katika utendaji kazi, kupata mbinu za kuwaongoza watendaji waliochini yao na hivyo kuwapunguzia msongo wa mawazo katika kuwaongoza pamoja na kuboresha ushirikiano na mawasiliano yenye tija baina yao na watumishi wanaowasimamia.

Hata Hivyo Mhandisi Mativila amewataka viongozi wa TANROADS kutoa mrejesho [feedback] kwenye jamii kwa kutangaza yale wanayofanya kwa kuzingatia kuwa Mheshimiwa Rais Samia anatoa fedha nyingi sana kutekeleza miradi kwani mtu hawezi kujua umefanya kitu gani bila kumwambia.

“Kuna kazi nyingi sana tunafanya hasa huko mikoani, Rais anatoa fedha nyingi sana tuweze kutekeleza miradi, hivyo ninawaomba mameneja wote mtoe taarifa za mara kwa mara kwa umma zinazohusiana na mnachotekeleza iwe unafanya matengenezo au ujenzi wa miundombinu mipya hizo Mrejesho [feedback] ufike kwenye jamii ionekane kazi inayofanyika vinginevyo jamii haitambui nini tunafanya inaweza ikadhani fedha zinapotea tu” ameongeza Mhandisi Mativila

Previous articleWATAALAMU WA MAABARA MWANZA WATAKIWA KUZINGATIA MIIKO YA KAZI ZAO
Next article‘BWAWA LA NYERERE LAFIKIA UJAZO WA MITA BILIONI 6 ZA MAJI – WAZIRI MAKAMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here