Serikali imefikisha Tani mia Saba za viwatilifu aina ya Salfa kwenye Chama kikuu Cha Wakulima mkoa wa Pwani CORECU kwaajili ya zoezi la usambazaji kwa Wakulima wa zao la korosho linaloendelea mkoani humo.
Akizungumza na baadhi ya Wakulima wa mkoa huo kwenye mnada wa Saba wa ufuta uliofanyika Katika ghala kuu la Wilaya ya Kibiti Meneja wa CORECU Mantawela Hamisi amesema maandalizi ya msimu wa zao la korosho wa mwaka 2023 yameanza ambapo Wakulima wameshaanza kupokea na kuanza kupulizia mikorosho yao Viwatilifu vyao aina ya Salfa ya unga na ya maji.
Amesema matarajio waliyonayo mkoa mzima wa Pwani kupitia Bodi ya Korosho Tanzania -CBT- na Chama hicho kikuu ni kupokea Tani 1000 ambazo zinaendelea kugaiwa kwa Wakulima kiwilaya na Kata kulingana na Wakulima walivyojiorodhesha kwenye mfumo kupitia Maafisa kilimo wao.
Amesema Tani 300 zingine bado hazijafika hivyo amewaomba Wakulima kuwa wavumilivu kusubiri kiasi hicho cha Salfa ambayo bado haijafika.
“Na zikifika zinapokelewa kwenye mfumo ndipo Watu wa Bodi ya Korosho Tanzania wanazichakata na kutoa maelekezo ya jinsi ya kugawana Salfa hiyo kulingana na mfumo unavyopanga”
“Yaani kadili Salfa zinavyoingia, ndivyo zinavyoingizwa kwenye mfumo na jinsi mfumo unavyogawa ndipo na sisi CORECU ndivyo tunavyowaletea Wakulima pembejeo zenu” amesema Hamisi.
Amesema usambazaji wa pembejeo hizo unaendelea katika mkoa mzima wa Pwani Hulu akionyesha malori yakipakia pembejeo hizo kuzipeleka katika Wilaya za kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo, Kibaha, Kibiti na Rufiji.
Hatahivyo Meneja huyo ameonyesha kushangazwa na mwitikio mdogo wa Wakulima kujisajili katika mfumo wa pembejeo kutoka katika Wilaya za Kibiti na Rufiji ambao ndio wamekuwa Wakulima wakubwa wa mazao ya ufuta na Korosho na kujisababishia kupata mgao mdogo wa pembejeo hizo tofauti na Wilaya ya Mkuranga ambayo Wakulima wake walijisajili kwa wingi hivyo wengi watapata pembejeo kuliko Wilaya zote za mkoa huo.
“Mkuranga wameitikia zaidi kuliko Kibiti na Rufiji ambapo Wilaya ya Kibiti kuna Wakulima wengi zaidi, msijemkashangaa usambazaji wa pembejeo Wilaya ya Mkuranga ikawa imepokea pembejeo nyingi kuliko Wilaya ya Kibiti kwasababu wenzetu waliitikia kujisajili lakini huku sijui mlikuwa mnaogopa nini?”
“Sasa madhara yake utasikia watu wana namba lakini hamjapata pembejeo ni kwakuwa hamkujisajili kwa wakati na muda umeshakwenda hivyo nyinyi mliokuwa mkijivuta vuta ntakuja kupewa baadae sana Sasa zikiisha tusijetukalaumiana”
Aidha Hamisi amesema pembejeo hizo serikali inazigawa kwa ruzuku ambapo mkulima hachangii kiasi chochote cha fedha lakini hazitatosheleza kila mkulima.
“Pembejeo hizo hazitatosheleza kila mkulima kwasababu pembejeo huletwa kwa namna mkulima alijisajili kwenye mfumo wa pembejeo”.
“Mfuko mmoja wa Salfa utapulizia kwenye miti mia ya mikorosho Sasa kama wewe una Miche mingi kuliko pembejeo ulizopewa maana yake ni kwamba pale serikali ilipoishia kukusambazia unaruhusiwa kwenda kujitafutia sehemu nyingine kwasababu serikali haiwezi kumuhudumia mkulima kwa mahitaji yake yote”
Pia amewataka Maofisa kilimo waliohusika katika kusajili Wakulima kwenye mfumo huo kwa kushirikiana na uongozi wa Amcos za Kata husika wahakikishe Wakulima wao wanapata pembejeo zao kama walivyojiandikisha.
Akizungumzia bei ya ufuta iliyopitishwa katika mnada huo kuwa ni shilingi 3805.34 kwa kilo moja.