Home KITAIFA TANESCO YAWACHARUKIA WAFANYABIASHARA MLANDIZI WANAOVUNJA SHERIA NA TARATIBU

TANESCO YAWACHARUKIA WAFANYABIASHARA MLANDIZI WANAOVUNJA SHERIA NA TARATIBU

Na Victor Masangu,Kibaha

Kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara ndogo ndogo kuamua kufanyia biashara zao chini ya nyaya kubwa za umeme hali ambayo inahararisha zaidi usalama wa maisha yao kwani kufanya hivyo ni kinyume kabisa na sheria na taratibu zilizowekwa.

Katika kuliona hilo na kulitafutia ufumbuzi suala hilo Shirika la umeme (Tanesco) Mkoa wa Kinondoni kusini limefanya ziara maalumu ya kutoa elimu na kuwataka baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la mlandizi na maeneo mengine Wilayani Kibaha kuondoa biashara zao ambazo wanazifanyia chini ya miundombinu ya Tanesco.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Kinondoni Kusini Lilian William wakati wa zoezi la kuwaondoa baadhi wafanyabiashara wa eneo la mlandizi sokoni ambao wamekuwa wakiendesha shughuli zao chini line kubwa za umeme.

“Tupo katika zoezi la kuwaondosha baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hili la mlandizi sokoni kwani wanafanya makosa kutokana na kufanya biashara chini ya miundombinu ya line kubwa ya umeme kwa hiyo hii ni hatare sana kwa usalama wao kwani nyaya zinaweza kukatika,”alisema Lilian.

Aidha afisa huyo alibainisha kwamba wafanyabiashara hao wanapaswa kutambua kuendesha shughuli zao chini ya line kubwa ya umeme wanaweza kusababisha madhara makubwa pindi litakapokuja tatizo la nyanya kukatika hivyo ni vizuri wakahama na kutafuta maeneo mengine.

“Sisi kama Tanesco tutaendelea kuwaelimisha wafanyabiashara kuachana kabisa na kufanya biashara zao na pia tutawaondosha wote maana hii line yetu kubwa ya umeme kutokea Dar es Salaam hadi morogoro tumebaini kuwepo kwa maeneo watu wanavunja sheria ya kupanga hata bidhaa zao,”alifafanua Lillian.

Katika hatua nyingine aliwataka kuhakikisha wafanyabiashara wote kuzingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa Upande wake msimamizi wa njia kuu za kusafirishia umeme kanda ya Dar es Salaam Juma Sungura alisema kuwa kwa sasa wamejipanga katika kuilinda miundombinu hiyo ya umeme ili kuepukaba na madhara ambayo yanaweza kujitokeza kwa wananchi.

Nao baadhi ya wananchi wanaoishi katika eneo la mlandizi Wilayani Kibaha walisema kuwa kufanya biashara chini ya nyaya kubwa za umeme ni hatari kwa maisha yao hivyo wanapaswa kutafutiwa maeneo mengine ambayo yatakuwa ni rafiki zaidi kwa biashara zao.

Previous articleWENYEVITI NA WAJUMBE WAJIUZULU KWA MADAI YA SERIKALI KUSHINDWA KUPELEKA UMEME KATIKA MAENEO YAO
Next articleTOZO MIAMALA YA SIMU KUFUTWA.. MUSWADA WATUA RASMI BUNGENI _ MAGAZETINI LEO ALHAMISI JUNI 22/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here