Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Wilaya ya Ulanga wanatarajia kufanya tamasha la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa anayofanya katika Wilaya hiyo ikiwemo utekelezaji wa miradi ya afya ,elimu pamoja na miundombinu .
Katibu wa hamasa na chipukizi UVCCM wilayani humo, Thomas Machupa amesema ,mpaka sasa katika mikopo ya asilimia 4 kati ya 10 kwa vijana ,wanawake na wenye ulemavu tayari Wilaya hiyo vijana ndio wanaoongoza kwa kunufaika.
Aidha katibu huyo wa hamasa amesema, zaidi ya vijana 2500 wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo Juni 10, mwaka huu.
Amesema tamasha hilo litapambwa na shughuli mbalimbali wilayani humo ikiwemo kufanya usafi katika hospitali ya Wilaya,kutenbelea wafungwa pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima Ukwama kwa ajili ya kutoa mahitaji maalumu.