Home KITAIFA TAKUKURU KAGERA YABAINI MAPUNGUFU KWENYE MIRADI YENYE THAMANI YA BIL.1.5.

TAKUKURU KAGERA YABAINI MAPUNGUFU KWENYE MIRADI YENYE THAMANI YA BIL.1.5.

 

Na, Denis Rutagwelela.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani kagera imesema kuwa miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya  shilingi bilioni 1.5  kati ya miradi 52 yenye thamani ya zaidi shilingi  bilioni 9.

 

Akitoa taarifa hiyo kaimu  mkuu wa Takukuru mkoani humo, Ezekia Sinkala wakati akizungumza na waandishi wa habari  amesema kuwa  ufuatiliaji huo ulifanyika  kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu na kubaini mapungufu hayo katika miradi ya kimaendeleo mkoani humo.

 

“Miradi  iliyobaibika kuwa na mapungufu  ni mradi wa barabara ya Nyakahanga -Nyabiyonza ulibainika  kutokuwa mifereji ya kupitisha maji,ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje zahanati ya buganguzi ulibainika kuwa na mapungufu kwenye gypsum ,vifaa vinavyonunuliwa havi ingizwi stoo pamoja na   ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari  na miradi ya maji walibaini kuwa masharti ya mikataba hayazingatiwi”

 

Sankala ameongeza kuwa kwa kipindi hicho wamepokea malalamiko 120  huku malalamiko 48 yakiwa ni malalamiko juu ya halmashauri ikifuatiwa idara ya afya 10,elimu malalamiko tisa , polisi tano na TANESCO 8 na kuwa kati ya malalamiko hayo  baadhi yamefanyiwa kazi na mengine yapo katika hatua mbalimbali.

 

 

Aidha amesema kuwa katika kipindi cha Jaruari-Machi 2023 wamefanikiwa kumkamata mfanyabishara Bw, Frank Kisanga mkazi wa Babati Manyara aliyeshawishi kutoa rushwa ya shilingi milion 10 kwa maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA katika kituo cha Forodha mpaka wa Mutukula wilaya ya Missenyi ili waachie mzigo wake wa magendo Box 12 zenye roller 36 za stika zinazotumika kubandika kwenye vinywaji mbalimbali kuonesha kuwa vimelipiwa kodi ambazo zilikuwa zinatoka nchini Uganda.

 

“Mzigo huo ulitoka Uganda na kuingizwa Nchini kwa njia sisizo rasmi baada ya Uchaguzi kufanyika tarehe 20/04/2023 watuhumiwa wawili ambao ni Bw, James Damian na Jacob John walifikishwa mahakama na kushitakiwa kwa kosa la kutoa rushwa shilingi milion 10 kinyume na kifungu 15 (1) b cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya namba 11 ya mwaka 2007(marekebisho ya mwaka 2022)”

 

Sankala aliendela kusema kuwa mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Missenyi mhe, Mayombo washitakiwa walikiri makosa yao Mahakama iliwatia hatia na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi laki 5 kila mmoja au kwenda jera mwaka mmoja ambapo washitakiwa walilipa faini hiyo na shilingi milion 10 zimetaifishwa kuwa mali ya Serikali.

 

Sambamba na hilo amesisitiza kuwa katika kipindi cha mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu TAKUKURU mkoani Kagera wamejiwekea malengo yakitekeleza vipaumbele ikiwa ni pamoja na kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za umma, kuelimisha umma kwa kutumia njia mbalimbali pamoja na kutatua kero kwenye jamii kupitia programu ya TAKUKURU RAFIKI

Previous articleSAMIA AFANIKISHA MUAFAKA KARIAKOO
Next articleRAIS SAMIA AONGEZA MILIONI 20 KILA GOLI LA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here