Home KITAIFA TAEC WATAKIWA KUWEKEZA ZAIDI UTAFITI KATIKA ENEO LA SAYANSI YA NYUKLIA

TAEC WATAKIWA KUWEKEZA ZAIDI UTAFITI KATIKA ENEO LA SAYANSI YA NYUKLIA

 

TUME ya nguvu za Atomiki nchini, imetakiwa kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupata bunifu nyingi hasa kwenye eneo la Sayansi ya Nyuklia kwani ni muhimu sana katika ulimwengu wa sasa wa teknolojia kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ,teknolojia na Ubunifu Prof Maulilio Kipanyula , leo Jijini Dodoma kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu wakati wa Siku ya Atomiki kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu iliyoambatana na maandamano yaliyofanyika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

TAEC mna kazi kubwa sana ya kuhakikisha mnafanya tafiti zaidi kwenye eneo la sayansi ya Nyuklia kwani karibia ulimwengu wote sasa umegekia huko na lengo ni kukuza uchumi wa nchi na naamini kupitia maonesho haya wananchi watapata nafasi ya kuijua zaidi tume hii,”

Na kuongeza kuwa “Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni moja ya taasisi muhimu sana katika taifa letu kwa sababu inagusa sekta nyingi sana ukianzia kwenye sekta Afya mionzi inatumika ,kwenye chakula,mbegu na maeneo mengine mengi hivyo ni muhimu sana kuongeza tafiti na wanachi waelimishwe zaidi kuhusu majukumu ya taasisi hii,”amesema Prof.Kipanyula

Previous articleWAMI-RUVU YAWAONDOA WACHAFUZI WA MAJI MTO MOROGORO
Next articleRAIS DKT. SAMIA AMUANDALIA DHIFA YA KITAIFA RAIS KAGAME

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here