Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Hamis Tabasam amezindua mashindano ya mpira wa miguu maarufu (Tabasam Cup 2023) ambayo yanashirikisha jumla ya timu 184 kutoka kata 26 za Jimbo hilo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo makubwa ya kiihistoria na ayajawahi kutokea kwa mkoa wa Mwanza katika ngazi ya majimbo Tabasam amesema, lengo lake ni kusaidia kukuza vijapi vya vijana katika Jimbo hilo.
Aidha amesema ametoa vifaa vya michezo mbalimbali kwa timu zote zinazoshiriki mashindano hayo huku akiahidi kutoa vifaa vingine vya michezo kwa timu ambazo zitashinda na kuingia ngazi ya tarafa, vifaa hivyo ni pamoja na viatu,jezi na zawadi nyinginezo nyingi.
Tabasam amesema, mashindano hayo timu itakayoibuka kidedea katika ngazi ya kata itajinyakulia zawadi ya ng’ombe mmoja na jumla ya ng’ombe 26 zimetolewa na mbunge huyo kwa ajili ya zawadi kwa timu zitakazoibuka kidedea.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amemshukuru mbunge wa Jimbo hilo Hamis Tabasam kwa kufanya mashindano hayo sambamba na kusema yataleta chachu katika Jimbo hilo na Halmashauri kwa ujumla pamoja na Wilaya hiyo.
“ Kupitia michezo hii, ni kumuenzi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa vitendo, mimi nakupongeza sana mheshimiwa mbunge, Ilani ya chama chetu cha mapinduzi tunayoisimamia pia imetutaka kuhakikisha michezo na yenyewe inapewa kipaumbele,Senyi Ngaga’Mkuu wa Wilaya Sengerema.