Serikali imeombwa kuendelea kuzishika mkono taasisi za kifedha kutokana changamoto inayowakabili wakulima katika masuala ya mikopo wengi wao wakilalamika kuchajiwa riba kubwa kwa baadhi ya taasisi hizo.
Afisa mauzo kampuni ya Agricom inayojuhudisha na uuzaji wa sana za kilimo, Mkali Crispo ametoa ombi kwa serikali mbele ya Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo David Silinde wakati wa maeneosho ya 30 ya Nanenane yaanayoendelea mkoani Morogoro.
Amesema mchakato wa ukopeshaji umekuwa ukichukua muda mrefu, masharti yanayowekwa hugeuka kikwazo kwa wakulima hali ambayo inawafanya kukosa uwezo wa kumiliki mashine hizo.