Home KITAIFA TAASISI YA MWALIMU NYERERE PWANI YAWAKUMBUKA WATOTO NJITI HOSPITALI YA MLOGANZILA

TAASISI YA MWALIMU NYERERE PWANI YAWAKUMBUKA WATOTO NJITI HOSPITALI YA MLOGANZILA

TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na baadhi ya wadau imetoa misaada kwa watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda (Watoto Njiti) waliolazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila.

Aidha imetoa misaada kwenye sekta ya elimu ili kuboresha mazingira ya usomaji na vifaa kwa wanafunzi wa baadhi ya shule Wilayani Kibaha.

Katibu wa Taasisi hiyo ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani Omary Punzi alisema kuwa wamefikia hatua hiyo ili kuendelea kutimiza malengo ya Taasisi hiyo ambayo ni mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na uamsikini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi huduma za tiba wa Hospital ya Mloganzila Dk Faraja Chiwanga alisema kuwa kuna sababu mbalimbali zinatajwa kuchangia hali hiyo ikiwa ni pamoja na magonjwa yasiyoambukiza na ukosefu wa lishe bora.

Naye mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kambarage Happynes Tesha alisema kuwa msaada wa mifuko 50 ya saruji iliyotolewa na taasisi hiyo itaongeza nguvu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea shuleni hapo.

Kaimu mkuu wa Shule ya Msingi Mtambani Sikitu Dibwe alisema kuwa msaada wa nguo za michezo walizopata kutoka kwenye taasisi hiyo utasaidia wanafunzi kucheza michezo ambayo ni sehemu ya kuchangamsha akili.

Misaada iliyotolewa ni pamoja na mafuta ya watoto, sabuni, saruji na mavazi ya michezo ikiwa ni sehemu ya kazi za taasisi hiyo kusaidia jamii.

Previous articleTAWA YAMWAGA MABILIONI BABATI, SHUGHULI ZA UTALII ZANEEMESHA WANANCHI
Next articleDKT. BITEKO AMTAKA MSAJILI WA HAZINA KUTOA MAELEZO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here