Watanzania watakiwa kudadisi na kujua umuhimu wa ulinzi wa taarifa binafsi za afya na kuhamasisha mabadiliko ya kisheria na sera za nchi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri Thamani Neema Lugangira ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Azaki za kiraia Tanzania ameyasema hayo wakati akitoa semina maalum kwa wahariri na waandishi wa habari kuhusu ulinzi wa taarifa binafsi za afya.
Lugangira alisema tatizo la ulinzi wa taarifa binafsi za wagonjwa na wananchi wa kawaida bado kunachangamoto japo baadhi ya watu wanaofika vituo vya afya na hospitali kuomba taarifa zao ,utumia muda mrefu baada ya kutibiwa na huwa hawapatiwi kwa wakati na wengine kunyimwa kabisa kutokana na sababu mbalimbali na kukatishwa tamaa.
Lugangira aliwaeleza wahariri na waandishi wa habari wajibu wa kundi hilo kuelimisha umma wa watanzania kuhusu umujimu wa taarifa za afya.
Kikao hicho kilichoudhuriwa na muwakulishi wa Transform Health kutoka nchini Kenya Beatrice Okechi alizishauri Serikali kutoa ushirikiano kwa wahitaji pindi wanapohitaji taarifa zao na kuondoa vikwazo ili wananchi wafuraie huduma wanazopatiwa katika vituo vya afya na hospitali.
Mbali na mafunzo hayo Taasisi hiyo ilifanikiwa kuzindua kikundi cha waandishi wa habari 15 kutoka mikoa mbalimbali.