Mkuu wa wilaya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi amelipongeza shirika la madini Tanzania (STAMICO) kupitia mgodi wa Kiwira_Kabulo Kwa kusaidia wananchi wanaouzunguka mgodi huo Kwa kuwapatia huduma jamii.
Mhge. Mgomi ametoa pongezi hizo Juni 8,2023 wakati wa ziara ya siku moja ya kutembelea migodi ya Kabulo na Kiwira yanakochimbwa makaa ya mawe ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya uzalishaji mkaa huo.
Mhe. Mgomi amesema licha ya mgodi wa Kiwira _ Kabulo kukumbwa na changamoto ya mda mrefu ya kutozalisha makaa ya mawe wamejitahidi kushirikiana na jamii inayowazunguka Kwa kuwasaidia kusogeza huduma za jamii.
Mhe. Mgomi amesema uwepo wa migodi hiyo umewanufaisha wakazi wa kijiji cha Kapeta kata ya Ikinga wilayani humo, kwa kujengewa huduma za jamii ikiwepo kujengewa kituo cha afya, kupelekewa huduma ya maji, kukarabati kituo cha Polisi, nyumba za watumishi na miundombinu ya mgodi.
“Niwapongeze Sana STAMICO Kwa uwekezaji wenu kwani mmeacha alama kubwa sana kusaidia hii jamii kwani hii ndo dhana ya serikali kutaka uwekezaji kama huu kusaidia wananchi wanaouzunguka maeneo yenye uwekezaji”,amesema Mhe.Mgomi.
Aidha Mhe.Mgomi amesema mpaka sasa uongozi wa Kiwira Coal Mining wapo kwenye hatua za kuanza ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya msingi Kapeta wilaya ya Ileje Ili kuondoa changamoto ya uchakavu wa vyumba vya madarasa.
Mratibu wa Mgodi wa makaa ya mawe Kiwira _Kabulo Peter Maha amesema wapo kwenye mazungumzo na shirika la umeme Tanesco juu ya mchakato wa uzalishaji wa umeme Megawati 200 Kiwira 1 na Megawati 300 Kiwira II kwa kuunganisha umeme huo kwenye gridi ya taifa.