Home KITAIFA SPIKA DKT. TULIA AMUONYA WAITARA

SPIKA DKT. TULIA AMUONYA WAITARA

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema kitendo cha Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara kuvua koti na tai akiwa ndani ya Bunge ni utovu wa nidhamu.

 

Dkt. Tulia ametoa kauli jana Mei 9, 2023 wakati akihitimisha kikao cha Bunge jijini Dodoma baada ya kusoma muongozo wa maswali ambayo baadhi ya wabunge hawakuridhika na majibu yake.

 

Spika Tulia amesema kitendo hicho kwa mujibu wa kanuni za bunge hakikibaliki ikiwemo vitendo vingine vya kupiga magoti na sarakasi ambavyo tayari alikwisha vikemea.

 

“Kitendo cha waitara kuvua tai na koti ndani ya bunge ni kulidharau na kushusha hadhi ya bunge hairuhusiwi na isijirudie tena kama una hasira kaanzie nje”

Previous articleAOZA VIDOLE KWA KUDUNGWA SINDANO YA UTI DUKA LA DAWA _ MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 10/2023
Next articleDKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here