Home KITAIFA SITA WASHIKILIWA NA POLISI SAME

SITA WASHIKILIWA NA POLISI SAME

 

Watu sita wanashikiliwa na Polisi wakituhumiwa kuficha Kwa kuwahifadhi wahalifu walioingia kinyemela na kujihusisha na uchimbaji wa madini eneo ambalo ni chanzo tegemeo cha maji kwa wakazi zaidi ya 22,000 wa kata nne za Vudee,Mwembe,Mhezi na Mbangalala Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao sita ni matokeo ya oparesheni ya kamati ya Usalama Wilaya ya Same iliyo ongozwa na mwenyekiti wake ambae ni mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni, waliolazimika kufanya msako kwa kushtukiza baada ya kupata taarifa za kuwepo watu zaidi ya 70 wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini aina ya Dhahabu bila vibali.

Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya ya Same taarifa zilizo mfikia ni kwamba mbali na wachimbaji hao kufanya shughuli zao kinyemela, pia wameharibu miundombinu ya maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji kwakua wanasafisha madini moja Kwa moja kwenye bwawa wakitumia Mercury ambayo ni hatari kwa binadamu.

Awali kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mteke Felix Ngeti amesema kwa sasa asilimia kubwa ya watu wamelazimika kuacha kutumia maji hayo kwakua uharibifu ni mkubwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kulazimika kutafuta huduma ya majisafi maeneo ya mbali.

Baadhi yao wakazi wanaoishi jirani na eneo hilo kulikofanyika uharibifu wamepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na kamati ya usalama, wakisema Hali ilizidi kuwa mbaya kwakua kumekua na ongezeko la idadi ya watu wanaotoka maeneo mbalimbali na kuingia kinyemela katika eneo hilo la chanzo cha Maji na kuanza uchimbaji wa madini.

Previous articleMAKALI YA MAISHA KUPAA BEI ZA MAFUTA ZAPANDA, WASAFIRISHAJI WAITANA WAPANDISHE NAULI_ MAGAZETINI LEO ALHAMISI AGOSTI 03/2023
Next articleBIASHARA YANGU IMEPAMBA MOTO BAADA YA KUFANYIWA DAWA HII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here