Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) tarehe 02 Aprili, 2023Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi, Ikulu, Dar es Salaam Aprili 02, 2023.Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene, Ikulu-Dar Aprili 02, 2023.