Home KITAIFA SIMBACHAWENE AWATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UONGOZI, TMDA YAPONGEZWA

SIMBACHAWENE AWATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UONGOZI, TMDA YAPONGEZWA

 

 

NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.

 

WANAWAKE nchini wametakiwa kujiunga na mafunzo ya uongozi kupitia programu maalamu inayotolewa na Taasisi ya uongozi iliyonzisha na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani.

 

Akizungumza jana tarehe 5/5/2023 Jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Taasisi ya Uongozi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa ni vizuri wanawake wakajiunga na mafunzo ya uongozi ili kuleta tija katika kuongeza idadi ya viongozi nchini.

 

“Kuna idadi ndogo ya wanawake katika safu ya uongozi nchini ni vizuri wakasoma mafunzo hayo ili kukuza vipaji vyao kwa ajili ya kuleta usawa katika utekelezaji wa majukumu” amesema Simbachawene.

Simbachawene amewapongeza wahitimu kwa kupata mafunzo ya uongozi jambo linakwenda kusaidia kufikia malengo tarajiwa katika kuwafikia wananchi kwa kutoa huduma bora.

 

Amewataka kwenda kuwa viongozi bora na kutumia vizuri talanta zao ili kuleta maendeleo kwa Taifa.

 

“Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema ili tuendelee tunaitaji mambo manne ambayo ni watu, ardhi, siasa safi pamoja na uongozi bora” amesema Simbachawene.

 

Amefafanua kuwa hali ambayo inawasukuma kuandaa viongozi bora kutokana na ongezeko la idadi ya watu, kwani matokeo ya sensa na watu mwaka 2022 inaonesha Tanzania ina jumla ya watu milioni 61.7.

 

Ameeleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu asilimia 3.2, hivyo kuna idadi kubwa ya watu “Tunaitaji viongozi bora makini kwa ajili ya kumudu kusimamia rasilimali za Nchi”.

 

Simbachawene amesema kuwa mafunzo ya uongozi ni muhimu, huku akiwataka wahitimu kuwa chachu ya mabadiliko katika maeneo yao ya kazi.

 

“Mkakuze utawala bora wenye kufata haki, kanuni, miongozo na taratibu, kuimarisha uwajibikaji na kuongeza uaminifu, kuimalisha utendaji wa kazi ili kumsaidia Rais ambaye amefungua milango mingi ya kimaendeleo” amesema Simbachawene.

Kwa upande wake Roberta Feruzi Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ambaye ni mhitimu wa mafunzo hayo ya uongozi amemshukuru mwajiri wake TMDA kwa kumpa fursa ya mafunzo hayo ya ngazi ya juu katika Uongozi.

 

“Mafunzo haya yamenijengea uwezo, maarifa na stadi za juu katika uongozi kimataifa. Ujuzi huu utaongeza chachu katika utendaji wangu wa kazi na hivyo kuleta tija katika ufanisi wa kazi. Utaboresha utendaji wa Taasisi na kusaidia kuharakisha maendeleo ya nchi kwa ujumla.” Amesema Roberta Feruzi.

 

Previous articleACT YATAKA FCC IJIUZULU SAKATA LA TANGA CEMENT , SERIKALI YAJIBU _ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MEI 06/2023
Next articleDKT. MPANGO ATUA NCHINI BURUNDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here