Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene amekiri kuwepo kwa mapungufu kwenye sheria ya likizo ya uzazi hasa kwa wanawake wanaojifungua watoto ambao hawajatimiza muda wake (Njiti) na kuwataka wabunge wapitie upya ikibidi ifanyiwe marekebisho.
Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Agnes Hokorororo leo Juni 14 bungeni jijini Dodoma mbae ameihoji Serikali kuhusu mpango wa kuongeza siku za likizo kwa wazazi wanaojifungua watoto njiti.
Simbachawene amesema siku 84 za likizo kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wake (Njiti ) bado hazitoshi kwani uumbaji huwa bado unaendelea hivyo akaomba maoni ya wabunge ili sheria hiyo ipelekwe bungeni na kufanyiwa marekebisho.