Home MICHEZO SIMBA SC MSIMU HUU HAITAKI KUFUNGWA WALA KUPOTEZA MCHEZO, VIONGOZI WATHIBITISHA

SIMBA SC MSIMU HUU HAITAKI KUFUNGWA WALA KUPOTEZA MCHEZO, VIONGOZI WATHIBITISHA

 

Na Dishon Linus

Uongozi wa Simba sc umeweka wazi kuwa, malengo yao msimu huu ni kushinda mechi zote watakazocheza kwenye ligi kuu na mashindano mengine, huku wakiweka rekodi ya kuwa timu isiyofungika.

Baada ya kupoteza taji la ngao ya Jamii, Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu wakibeba mara mbili wameweka wazi kuwą malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanatetea mataji yote ambayo walibeba msimu uliopita na wanaendelea kuyashikilia.

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, watashinda mabao mengi kwenye kila mchezo na hawataruhusu bao lolote kwenye mechi hizo zinazofuata.

“Tunasikitika kuwa, tumecheza mechi mbili za ligi mpaka sasa na kufunga mabao sita tu na kuruhusu mabao mawili hili ni jambo ambalo hatuwezi kulifurahia”.

“Kwa namna ambavyo timu yetu ilivyo na wachezaji bora na wakali zaidi barani Afrika, ilipaswa tuwe tumefunga mabao mengi sana na kutoruhusu bao lolote tumeshinda mabao sita na kuruhusu mawili,Kocha wetu na wasaidizi wake, wanakwenda kurekebisha hilo tunataka kuwa klabu iliyofunga mabao mengi na kufungwa mabao machache,” amesema Ahmed.

Simba SC waliwachapa Mtibwa Sugar 4-2 pale Manungu Morogoro kwenye mchezo wa kwanza na kisha kuwachapa Dodoma Jiji FC mabao 2-0 kwenye mechi ya pili iliyochezwa Uwanja wa Uhuru.

Previous articleCOSTECH YAJA NA MBINU MPYA KUMALIZA TATIZO LA MATOKEO MABAYA SOMA LA HISABATI
Next articleTMDA YATOA TAHADHARI UTUPAJI HOLELA WA DAWA ZINAZOBAKI MAJUMBANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here