Home KITAIFA SIMBA ALIYEKUWA ANAKULA MIFUGO IRINGA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

SIMBA ALIYEKUWA ANAKULA MIFUGO IRINGA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

 

Na Dishon Linus_Iringa

Kikosi Cha kutafuta simba waliokuwa wakisumbua wananchi wa mkoa wa Iringa,katika moia ya wilaya ya kilolo kikosi hicho Cha utafutaji wa Simba kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Hifadhi (TAWA) na TAWIRI kilichokuwa kijiji Cha ilamba wilaya ya Kilolo Jana jumapili julai 16,2023 wamefanikiwa kumuua Simba mmoja dume ambaye aliemshambulia askari na kumjeruhi wakati akijaribu kumlaza usingizi ili arudishwe Hifadhini ndipo alipo mjeruhi askari huyo.

Kwa upande afisa uhusiano wa (TAWA),Vicky Kamata amesema “Simba hawa walikuwa wawili ambapo mmoja alikimbia akabaki mmoja, katika harakati za kumchoma sindano ya usingizi ndipo alipo mshambulia askari wetu CR Charles Mafuru na kumjeruhi kichwani na kwenye mkono.

“Wakati hayo yakifanyika ilitulazimu kumpiga risasi ya moto simba huyo baada kuona anamuangusha afande wetu na amekaa juu yake akijiandaa kumshambulia shingoni na kutaka kumuua, baada ya askari kumuua Simba walimkimbiza mgonjwa Charles hospitali ya wilaya ya Kilolo ambako alipewa matibabu na kuruhusiwa na hali Yale inaendelea vizuri kabisa”.

Aidha afisa huyo Vicky alisema zoezi la kuwasaka Simba hao linaendelea ambapo siku ya jana Jumamosi zilionekana alama za Simba na mtoto wake eneo la Ihemi ufatiliaji ulibaini kuwa wameelekea Ifunda wilaya ya Mufindi.

Previous articleNAIBU WAZIRI NDERIANANGA ATETA NA WANAFUNZI WA WERUWERU
Next articleRPC MOROGORO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MVOMERO WATAKIWA  KUSIMAMIA MIFUMO YA SHERIA KWA ASKARI WANAOENDA KINYUME NA MAADILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here