Home KITAIFA SHULE YA MAFUNZO YA JESHI RTS KIHANGAIKO YATAMBUA UMUHIMU WA WAKAZI WANAOPAKANA...

SHULE YA MAFUNZO YA JESHI RTS KIHANGAIKO YATAMBUA UMUHIMU WA WAKAZI WANAOPAKANA NA MAENEO YAO KWA KUTOA HUDUMA YA MATIBABU NA CHAKULA

Zaidi ya kaya 60 katika kijiji cha Pongwe Msungura Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa pwani wamepata huduma ya matibabu pamoja na chakula kwa makundi maalumu yaliyotolewa na shule ya mafunzo RTS Kihangaiko ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya jeshi hilo na raia.

Afisa habari wa shule ya mafunzo RTS Kihangaiko kapteni Fadhila Nayopa amesema, uimarishaji wa mahusiano hayo yanafanywa kila wakati pindi kuruti wanapomaliza mafunzo katika maeneo wanayopakana na wakazi hao.

Aidha kapteni Fadhila Nayopa amewataka wakazi hao kuacha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji katika maeneo ya mafunzo.

Kwa upande wao wakazi wa eneo hilo wamesema ushirikiano baina yao na jeshi hilo umekuwa na manufaa makubwa hasa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Previous articleNEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO UDIWANI KATA 14 _ MAGEZITINI LEO ALHAMISI JUNI 15/2023
Next articleDC MOMBA ATOA AGIZO KUMALIZA KERO YA FOLENI YA MALORI MPAKA WA TUNDUMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here