Home MICHEZO SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU BRAZIL LIMEMUONDOA ANTONY KWENYE KIKOSI CHA TIMU...

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU BRAZIL LIMEMUONDOA ANTONY KWENYE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA

 

Na Dishon Linus

Kutokana na tuhuma ambazo zinamkabiri winga wa Manchester United raia wa Brazil Antony shirikisho la mpira wa miguu limetoa tamko la kumuondoa mchezaji huyo kwenye kikosi cha timu ya taifa ili kupisha uchunguzi wa jambo hilo.

“Kwa kuzingatia ukweli uliojitokeza Jumatatu kuhusu mchezaji wa Manchester United Antony, ambao lazima uchunguzwe, na ili kumlinda mwathiriwa, mchezaji, timu ya taifa ya Brazil na CBF, shirika linaarifu kwamba mchezaji huyo kuondolewa katika timu ya taifa ya Brazil”.

Ikumbukwe hii inakuwa kesi ya pili ya mchezaji kutoka Manchester United kuhusu kuwapiga wapenzi wao, sakata ka Greenwood ambalo limemfanya aondolewe kabisa katika kikosi Cha united na sasa anawatumikia Getafe ya nchini Hispania.

Previous articleAWESO ASISITIZA KUPATA MAJIBU NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA MAJI KWA WAKATI
Next articleTUFANYE KAZI KWA USHIRIKIANO ILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here