Home KITAIFA SHIRIKA LA TMFD LAINGIA MAKUBALIANO YA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NA SHIRIKA...

SHIRIKA LA TMFD LAINGIA MAKUBALIANO YA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NA SHIRIKA LA MYCN

 

Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) leo April 5, 2023 limeingia kwenye makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja na shirika la Mwanza Youth and Children Network(MYCN) katika maeneo ya jinsia, haki za binadamu, afya na uezeshwaji wa jamii.

 

Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amesema kuwa, hatua hiyo ni hatua muhimu kwa kuwa TMFD inafanya kazi nyingi zinazoendana na shughuli zinazotekelezwa na MYCN hivyo makubaliano hayo yataongeza nguvu ya utendaji na utafutaji wa matokeo bora ya miradi.

 

Naye Mwenyekiti mtendaji wa shirika la MYCN Bwana Brightius Titus amesema kuwa, makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja yataleta ufanisi kwenye kutekeza vyema malengo ya mipango iliyowekwa kwa mashirika yote mawili na kupunguza changamoto za watoto na vijana.

 

Moja ya makubaliano hayo ni kutafuta miradi kwa pamoja, kutekeleza miradi, kufanya tathimini ya miradi na kutoa taarifa ya miradi kwa pamoja.

 

Makubaliano hayo yamefanyika kwenye ofisi za MYCN zilizopo Jijini Mwanza.

Previous articleWAZIRI MKUU: TANZANIA KINARA MASUALA YA MAAFA
Next articleRAIS DK.MWINYI APOKEA TUZO YA VIP GLOBAL WATER CHANGEMAKERS AWARD 2023, KUIFANYA ZANZIBAR KUWA NCHI YA KWANZA KUANDAA PROGRAMU YA UWEKEZAJI WA MAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here