Home KITAIFA SHIRIKA LA HAKI YANGU FOUNDATION LAZINDULIWA RASMI

SHIRIKA LA HAKI YANGU FOUNDATION LAZINDULIWA RASMI

Shirika jipya lisilo la kiserikali la HAKI YANGU FOUNDATION limezinduliwa rasmi leo katika ukumbi wa African Dreams Mkoani Dodoma na litajikita katika miradi ya kutetea na
kusaidia wanawake na watoto wenye uhitaji Nchini hasa katika Mkoa wa Shinyanga
kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi muasisi na mkurugenzi wa shirika hilo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA, Bi. Salome Makamba ametumia fursa hiyo kubainisha malengo ya shirika kuwa ni kusaidia jamii katika masuala ya kisheria, kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Haki Yangu amesema
Mkoa wa Shinyangani moja ya eneo litakalofikiwa sana huku baadhi wa wadau
waliohudhuria uzinduzi huo wakipongeza juhudi hizo.

 

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya shirika la Haki Yangu Bwana Richard Haule amesema Mkoa wa Shinyanga ni moja ya eneo
litakalofikiwa na ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa ushirikiano pindi shirika hilo
litakapowafikia.

 

Uzinduzi wa Shirika la Haki Yangu umehudhuriwa na viongozi wa serikali ,vyama vya siasa na wadau mbalimbali huku Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Felista Njau pamoja na Mbunge wa CCM jimbo la Kasulu Vijijini Mhe. Vuma Agustine wamepongeza upunifu na hatua aliyoifanya
Mhe. Salome Makamba katika kusaidia na kutetea haki za wanawake na watoto ili
kupunguza au kumaliza kabisa ukatili uliopo katika jamii

 

Previous articleDIRA YA MAENDELEO YAIBADILISHA NCHI ◾ UMASKINI WAPUNGUA ,KASI YA UCHUMI, UMRI WA KUISHI VYAONGEZEKA : MAGAZETINI LEO JUMANNE APRILI 04/2023
Next articleDITOPILE AGAWA FUTARI KONDOA, ASISITIZA KUIOMBEA NCHI NA KUMUOMBEA RAIS SAMIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here