Home KITAIFA SERIKALI YATIA SAINI MRADI WA B.800 UENDELEZWAJI JIJI LA DAR ES SALAM

SERIKALI YATIA SAINI MRADI WA B.800 UENDELEZWAJI JIJI LA DAR ES SALAM

KATIKA jitihada za kuboresha Miundombinu mbalimbali ya Jiji la Dar es salam Serikali imetia saini mradi wa uendelezaji wa Jiji hilo kwa Awamu ya pili ambapo utagarimu kiasi cha shilling Billion 800.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa uendelezaji jiji la Dar es Salam awamu ya pili leo jijini Dodoma, Mratibu wa miradi ya Benki ya Dunia ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI na TARURA Eng Humphrey Kanyenye amesema fedha hizo zimewekewa kipaumbele kwenye Miundombinu ya barabara,Masoko na uondoshaji wa taka ngumu zinazozalishwa kwenye masoko.

Akishuhudia utiaji saini huo, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Angellah Kairuki amewataka wakandarasi hao waliotia saini kutekeleza mradi kwa wakati.

”Tunategemea mtajifunza katika awamu ya kwanza na sitegemei kuona makosa ya kwanza yanajirudia mjueee mmekopaaa tuna imani mradi huu utaenda kwa wakati na utamalizika kwa wakati mtakapoenda kinyume tutarudi kwenye mkataba unavyosema”amesema Kairuki

Nae Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam Faustine Ndungulile akatoka wito kukamilishwa awamu ya kwanza ya DMP ili kuondoa vikwazo vitakavyopelekea kutokamilika kwa awamu hii ya Pili.

”Nimesikia maneno mengi nyuma ya pazia lakini naomba niwaombe Mawaziri pamoja na Makatibu kuna vikwazo vya DMP ya Awamu ya kwanza kuna mambo hayajakamilika naomba niseme visimamie visilete vikwazo kwa mradi huu wa Awamu ya Pili”amesema Ndungulile

Utekelezaji wa mradi huo utaanza April mwaka 2024 ambapo asilimia 74 ya fedha zitatumika kukarabati barabara, mifereji, maeneo ya wazi, masoko, vituo vya mabasi, kurekebisha miundombinu ya taka ngumu, kujenga uwezo kwa halmashauri hizo.

Previous articleMIL.18.6 ZATUMIKA KUKARABATI MADUKA YA UWT YALIYOTEKETEA KWA MOTO NJOMBE
Next articleWAZIRI UMMY APONGEZA UMEME WA UHAKIKA VITUO VYA AFYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here