Home KITAIFA SERIKALI YASEMA ITAENDELEA KUWAUNGA MKONO WADAU WA SEKTA BINAFSI

SERIKALI YASEMA ITAENDELEA KUWAUNGA MKONO WADAU WA SEKTA BINAFSI

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwaunga mkono wadau wa sekta binafsi katika jitihada zote za kuimarisha ustawi wa watoto wa Tanzania.

Amesema kuwa Serikali kwa upande wake imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na ustawi na afya ya mtoto sambamba na kuimarisha upatikanaji wa huduma za elimu kwa watoto wenye ulemavu hapa nchini.

Ameyasema hayo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2023) baada ya kushiriki mbio hizo za hisani zilizoandaliwa na benki ya Maendeleo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo ameisisitiza jamii ishiriki katika ulinzi wa watoto wenye ulemavu kwa kutoa taarifa kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya watoto hao.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imehakikisha hospitali zote za wilaya zinatoa huduma za watoto wachanga ikiwemo huduma ya mama kangaruu (Mother Kangaroo) kwenye vituo vya afya nchini. “Hii ni huduma maalum ya kutunza watoto njiti na wale waliozaliwa na uzito mdogo”

“Serikali inatekeleza utoaji wa huduma ya kumsaidia mtoto mwenye usonji ili aweze kuongea (speech therapy) pia kutoa huduma ya kumsaidia mtoto ili aweze kufanya matendo mbalimbali (occupational therapy)”

Previous articleRAIS SAMIA AYAPIGIA DEBE MASHIRIKA YA NDEGE AFRIKA KUBEBA VIFURUSHI _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI SEPTEMBA 03/2023
Next articleWAFUGAJI WATAKIWA KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here