Home KITAIFA SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUTUMA NYARAKA ZAKE KWA NJIA YA WHATSAPP

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUTUMA NYARAKA ZAKE KWA NJIA YA WHATSAPP

 

Serikali imepiga marufuku kwa watumishi wa umma kutumiana au kuwasilisha nyaraka za serikali kupitia mitandao ya kijamii ikiwamo whatsapp

Akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum Janejelly James Ntale alihoji uhalali wa matumizi ya makundi ya whatsapp kutumiana nyaraka za serikali, naibu waziri ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa Umma na utawala bora Ridhiwani Kikwete amesema Sheria inayosimamia nyara za serikali inaelekeza wazi kwamba mawasiliano yaserikalini yafanyike kwa njia ya barua lakini pia haielekezi vinginevyo

‘’nataka nilielekeze Bunge lako mhe Mwenyekiti haitakuwa sawa na nimarufuku ya serikali kuwasilisha au kutumiana document za kiserikali kupitia njia ya whatsapp na njia nyingine zisizokuwa rasmi isipokuwa kwa yale maelekezo ambayo yatakuwa yametolewa vinginevyo katika mamlaka,’’amejibu naibu waziri Kikwete,’’.

Previous article“TANZANIA IMEFANIKIWA KUTOKOMEZA MARBURG KUTOKANA NA UONGOZI MAHIRI WA RAIS SAMIA”- UMMY
Next article“WATOTO WAPELEKWE JANDO LA ZAMANI NA SI LA KISASA ILI WAKIOA WAJUE CHANGAMOTO ZA NDOA” _GWAJIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here