Home KITAIFA SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA FEDHA KUJENGA STENDI KAMSAMBA, IKANA MOMBA.

SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA FEDHA KUJENGA STENDI KAMSAMBA, IKANA MOMBA.

 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deo Ndejembi, ameahidi Serikali kuendelea kutafuta na kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya mabasi katika Kata za Ikana na Kamsamba Momba mkoani Songwe ikiwa ni hatua za kuboresha huduma ya usafiri pamoja na usafirishaji na kuinua uchumi wa Halmashauri ya Momba.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. Deo Ndejembi Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Momba mkoani Songwe Mhe. Condester Michael Sichalwe.

Mbunge Condester alitaka kujua mkakati wa Tamisemi kuwajengea kituo cha mabasi wananchi wa Momba katika Kata ya Kamsamba kwa ukanda wa chini na Kata ya Ikana kwa ukanda wa juu kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa vituo hivyo hasa kwa Wilaya hiyo ambayo pamoja na mengineyo lakini inaunganisha mkoa wa Songwe na Rukwa.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ndejembi amempongeza Mhe. Condester kwa kuwa mfuatiliaji jambo hilo akisema Serikali itaendelea kutafuta fedha na kutenga bajeti ili kujenga vituo hivyo ambavyo pia vitakuwa chanzo cha mapato katika Halmashauri ya Momba mkoani Songwe.

Previous articleTETE FOUNDATION YAADHIMISHA SIKU YA HEDHI DUNIANI KATIKA SHULE YA AMANI, MVOMERO MOROGORO
Next articleBANDARI YA DAR ES SALAAM YAWEKA REKODI MPYA KATIKA KUHUDUMIA SHEHENA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here