Home KITAIFA SERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI MBOLEA BORA NCHINI

SERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI MBOLEA BORA NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa MboleaTanzania(TFRA)Dkt.Stephan Ngailo amesema watahakikisha wanaongeza na kuimarisha upatikanaji, uzalishaji na usambazaji wa mbolea bora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Ameyasema hayo jijini Dodoma julai 17,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na muelekeo kwa mwaka 2023/24.

Dkt. Ngailo amesema kuwa dhima ya TFRA ni kuhakikisha upatikanaji, ufikiwaji, uwezo wa kumudu na ubora wa mbolea na visaidizi vyake kwa wakulima wote kwa njia ya udhibiti wa shughuli za mbolea kwa ajili ya uendelevu wa uzalishaji wenye tija katika kilimo.

“TFRA inashirikiana na sekta binafsi kuimarisha upatikanaji
wa mbolea bora inayozalishwa na kuingizwa nchini na kupanua mtandao wa usambazaji Kuendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji

Sambamba na kuratibu na kusimamia utekelezaji wa utoaji wa mbolea ya ruzuku,Kuratibu upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini (tani850,000),Kuendelea kudhibiti ubora wa mbolea,Kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea nchini,Kushirikiana na wadau kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea,Uimarishaji wa maabara ya uchambuzi wa mbolea,”amesema

Kadhalika ameeleza kuwa kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

Previous articlePPRA KUENDELEA KUWAFUNGIA WAZABUNI WANAOKIUKA SHERIA NA TARATIBU ZA MANUNUZI
Next articleEWURA: NCHI INA MAFUTA YA KUTOSHA NA MELI ZENYE SHEHENA YA MAFUTA ZINAENDELEA KUINGIA NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here