Serikali imewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Tanga na maeneo ya jirani kusudio lake la kukiboresha kiwanja cha ndege cha Tanga na hususani katika jengo la abiria, maegesho ya ndege na eneo la kuruka na kutua ndege ili kuendana na mahitaji ikiwemo kuruhusu ndege kubwa kutua
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema hayo baada ya kutembelea Kiwanja hiko, kufanya ukaguzi na kujionea uhitaji wa marekebisho uliopo
“Ukiangalia tumekaa kwa kipindi kirefu hakujawahi kufanyika mabadiliko yoyote katika Airport hii hivyo Rais Samia ameona ni muhimu kufungua Mkoa wa Tanga kwenye upande wa usafiri wa anga kwa kuhakikisha ndege kubwa zinatua hapa na uwepo wa Airport ya kisasa ndani ya Jiji la Tanga”
Naibu Waziri huyo amesema uboreshaji wa kiwanja hiko, utaenda sambamba na mahitaji ya sasa na fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Tanga ikiwa ni pamoja na fursa zala uwekezaji wa bomba la mafuta ambalo litaongeza idadi ya wageni watakaohitaji kutumia usafiri wa aina mbalimbali ukiwemo usafiri wa anga.