Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kuwawezesha wakulima kufikiwa na pembejeo za kilimo kwa wakati, kusafirisha mazao viwandani pamoja na masoko.
Waziri Kijaji amesema hayo mkoani Morogoro baada ya kutembelea wakulima wa miwa na wasambazaji wa pembejeo za kilimo katika Maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki na kubainisha hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kufanywa na serikali katika kuongeza ufanisi katika sekta za viwanda, biashara na kilimo.
Awali wakulima na wasambazaji hao wakabainisha namna wanavyokabiliwa na changamoto ya usafirishaji ikiwemo kukosekana kwa usajili wa barabara kutoka TARURA.