Home KITAIFA SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI MOJA KWA AJILI YA UKARABATI WA MASOKO TEMEKE

SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI MOJA KWA AJILI YA UKARABATI WA MASOKO TEMEKE

Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bil.1 kwaajili ya kufanya ukarabati wa masoko ndani ya Manispaa ya Temeke kwa lengo la kuboresha mazingira ya masoko wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Matinyi wakati akikagua Maendeleo ya Ujenzi wa soko jipya la kisasa ameridhishwa na hali ya ujenzi wa soko jipya na la Kisasa la Mbagala Kibonde Maji (Zakhiem) ambapo akimtaka mkandarasi wa soko hilo kulikabidhi kwa Manispaa ya Temeke ifikapo Agosti 15 ,2023.

Amesema ukarabati huo utafanyika sambamba na kufanya usafi katika masoko hivyo wamejipanga kuanzisha kampeni ya usafi ndani ya Manispaa ya Temeke itakayoanza hivi karibuni na kutekelezwa usiku na mchana.

Matinyi amesema Wafanyabishara wanaokaa pembezoni mwa barabara si wa Dar es Salaam pekee bali nchi nzima wanakua sawa na uchafu kutokana na kuzagaa hovyo barabarani.

Aidha amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Bil.2.843 ambazo zimejenga soko hili jipa na la kisasa ndani ya Manispaa ya Temeke.

Matinyi alisema baada ya Mkandarasi kukabidhi soko hili kazi inayobaki ni kwa Mkurugenzi Elihuruma Mabelya wa Manispaa ya Temeke, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdalah Mtinika pamoja na Katibu wa wafanya biashara katika soko hili.

“Wakae pamoja na kupanga namna Wafanyabishara watakavyo pangwa ndani ya soko huku kipaumbele kikiwa ni kwa wale wafanyabiashara ambao walikuwepo awali wakati wa lile soko duni la awali” amesema

“Viongozi mtatakiwa kusimamia mgawanyiko wa vizimba vya biashara kulingana na ukubwa wa biashara zao na jumla ya mamalishe 20 waliokuwepo awali watapewa kipaumbele ndani ya soko hilo” amesema Mheshimiwa Matinyi.

Amesema kuwa ujenzi wa soko hilo umechukua muda wa mwaka mmoja kikamilifu ambapo awali kulikua na soko duni ambapo hivi sasa kuna vizimba 160 hukumiundo mbinu ikiwa ni rafiki na kufikika kwa urahisi kwa ujumla.

Katika soko hili kutakua na ofisi za Manispaa ambao watasimamaia masuala ya msingi ndani ya soko pia kutakuwa na kitengo cha Tehama ambacho kitafunga mitambo maalumu ili kufuatilia nyendo zote za wafanyabiashara na utendaji wao kazi ndani ya soko.

Hatahivyo Matinyi ametoa onyo kali kwa kuahidi kuwachukulia hatua kali Wafanyabishara ambao watafanya uhuni endapo watapangishwa kwa fedha ndogo ya serikali halafu na wao wapangishe wafanyabiashara wengine.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema kuwa wamejipanga kuwaondoa wafanyabiashara ambao huzagaa hovyo pembezoni mwa barabara kwa kuwa wanakwenda kinyume na sheria huku akisisitiza kwa kusema kuwa Manispaa hiyo wamejipanga na wataanzisha kampeni ya kuwaondoa pamoja kuiweka Temeke safi kwa ujumla.

Previous articleMASHUJAA WALIOPOTEZA MAISHA VITANI WAKUMBUKWA MOROGORO
Next articleDC, MALISA, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA KIJIJI CHA SHAMWENGO NA KUZIPATIA MAJIBU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here