Home KITAIFA SERIKALI IMESHAURIWA KUTILIA MKAZO KILIMO IKOLOJIA

SERIKALI IMESHAURIWA KUTILIA MKAZO KILIMO IKOLOJIA

 

Tanzania Imeungana na Mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani huku Serikali ikishauriwa kuweka mazingira Rafiki kwa vijana ikiwemo kuwawezesha mtaji ili kuendana na kilimo ikolojia.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa jukwaa la Vijana Wilaya ya Chamwino lilopo chini ya Shirika lisilo la Kiserikali la Action aid Tanzania Magreth Malogo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambapo Kitaifa yanafanyika Agosti 12,2023 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Makundi ya Vijana kutoka maeneo mbalimbali Nchini.

Malogo amesema kwakuwa kilimo ikolojia kimekuwa ni uti wa mgongo kwa Vijana wasasa hivyo Serikali inajukumu la kuweka kipaumbele kilimo hicho ili kupunguza tatizo la ajira nchini na kukabiliana mabadiliko ya tabia ya nchi.

‘’Kama vijana tunaiomba serikali hii ya awamu ya sita itusaidie kwa kuwa Kilimo ikolojia ndio kimekuwa uti wa Mgongo kwa Vijana wa sasa ,kwa sababu saivi kuna tatizo kubwa la ajira, na vijana walio wengi tumeshajikita kwenye kilimo, Serikali iweze kukipa kipaumbele kilimo ikolojia ili tusiweze kuharibu mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ,pia tuweze kuhifadhi mazingira yetu, ili tuweze kupata uoto wa asili,’’amesema Malogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mwiga Mbesi amebainisha kuwa Serikali Imekamilisha Mapitio ya Muongozo wa Stadi za Maisha kwa Vijana utakaotumika kuwajengea Uwezo na kuwawezesha kukabiliana na changamoto ya Ajira.

Ameendelea kusema mapitio ya Mwongozo huo yamekamilika na kinachosubiriwa ni kusainiwa ili uanze kutumika.

Agosti 12 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani,Maadhimisho ya Mwaka huu yanaenda sambamba na Kaulimbiu kuwa “Kuelekea 2030 Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo endelevu”

Previous articleWAJASIRIAMALI WASOMI TUNDUMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA UWEZESHAJI KIUCHUMI
Next articleWAZIRI MKUU AGEUKA MBOGO UCHELEWESHAJI MAFAO YA WASTAAFU _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI AGOST 13 /2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here