Home KITAIFA SEKTA YA MADINI KUONGEZA MCHANGO WAKE KWENYE PATO LA TAIFA MWAKA WA...

SEKTA YA MADINI KUONGEZA MCHANGO WAKE KWENYE PATO LA TAIFA MWAKA WA FEDHA 2023/24

Wizara ya Madini imedhamiria kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa katika Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko Juni 23, 2023 alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Shirikisho Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini zinazofanywa na wachimbaji hao jijini Dodoma.

“Shabaha ya Wizara ya Madini Mwaka wa Fedha 2023/24 ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuwainua wachimbaji wadogo waweze kukua na kufanya vizuri katika uchimbaji,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, amewataka wachimbaji wadogo nchini kushirikiana katika shughuli za uchimbaji wa madini ili kukuza uchumi wao na kuongeza mchango wao katika Pato la Taifa.

Kikao hicho kifupi kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Katibu Mtendaji Tume ya Madini Eng. Yahya Samamba, Kamishna wa Madini Dkt. Abdul Rahman Mwanga na Watendaji wengine wa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Previous articleUJENZI WA BOMBA LA GESI KUTOKA BANDARINI HADI KIWANDA CHA ORYX KIGAMBONI WAKAMILIKA
Next articleADO SHAIBU: CCM ISIHODHI MCHAKATO WA KUPATIKANA KWA TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA MPYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here